Ndugu wateja, Unaweza kubofya katika jina la mkoa husika hapo chini kupata ratiba ya mgao wa umeme kwa baadhi ya mikoa:-
Tunawasihi wateja wetu na wananchi kwa ujumla kuwa na subira wakati jitihada zinafanywa kukabiliana na mgawo huo wa dharura
Pages
▼
November 30, 2010
November 29, 2010
MGAO WA DHARURA KWA MIKOA ILIYO KATIKA GRIDI
Kufuatia kutokea kwa hitilafu za kiufundi kwa baadhi ya mashine katika mitambo ya Songas, Ubungo na kuisha kwa mafuta katika mtambo wa IPTL shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limelazimika kufanya mgawo wa umeme kwa mikoa iliyoungwa katika gridi ya taifa.
Aidha, mitambo ya New Pangani na Kihansi nayo imepunguza uzalishaji kutokana na kupungua kwa kina cha maji.
Kutokana na hali hiyo Shirika limelazimika kufanya mgawo wa dharura ambao huenda ukaisha wakati wowote kuanzia wiki ijayo kutokana na jitihada zinazofanywa kunusuru hali hiyo kuendelea.
Miongoni mwa jitihada zinazofanywa ni kutengeneza kwa mashine hizo haraka na kukamilisha taratibu za kununua mafuta kwa ajili ya kuendesha mtambo wa IPTL. Hata hivyo, taratibu za kununua mafuta zinatarajiwa kukamilika wiki hii ili Jumatatu mafuta yaweze kupatikana haraka na kupelekwa IPTL kwa ajili ya kuendesha mtambo huo.
Ratiba ya mgawo inatarajiwa kutolewa baadaye na tunawasihi wateja wetu na wananchi kwa ujumla kuwa na subira wakati jitihada zinafanywa kukabiliana na mgawo huo wa dharura.
Badra Masoud,
MENEJA MAWASILIANO.
November 26, 2010
HUDUMA YA MAUZO YA LUKU YA MaxMalipo
Unaweza kununua umeme ukiwa mahali popote nchini Tanzania kwa kuwa mtandao huu umesambaa kila mahali. Ni rahisi pia kutumia kwani mteja anahitaji kujua namba yake ya mita tu ili kununua umeme. POS imesambazwa katika maduka ya kawaida hivyo basi huduma ya LUKU sasa inapatikana jirani na nyumbani au kazini kwako.
Hakuna gharama ya ziada unaponunua umeme kwa kutumia POS za MaxMalipo kwa hiyo unaweza mnunulia ndugu au rafiki aliye mbali nawe.
VITUO VYA MAX MALIPO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuwaomba radhi wateja wake na wananchi kwa ujumla kutokana na kukosekana kwa umeme katika baadhi ya maeneo nchini kutokana na kuharibika kwa baadhi ya mitambo jana asubuhi Jumanne Novemba 23, 2010.
Bila kutarajia baadhi ya mashine katika mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi wa Ubungo, Songas na Kidatu zilipata hitilafu ya kiufundi na kusababisha umeme uliozalishwa kutotosheleza mahitaji.
Upungufu huo ulisababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme kuanzia asubuhi saa nne hadi saa nne usiku kwa tarehe iliyotajwa hapo juu.
Hata hivyo, Shirika linaendelea na juhudi za kutatua hali hiyo ili kusiwepo na mgawo wa umeme.
Miongoni mwa jitihada zinazofanywa ni pamoja na kutumia mitambo yote ya kuzalisha umeme iliyopo kwa kiwango cha juu.
Wakati huo huo Shirika linapenda kuwatoa hofu wateja wote wa umeme wanaotumia LUKU kwamba hakuna tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo isipokuwa kuna baadhi ya vituo vya LUKU ambavyo vimeishiwa na LUKU na badala yake wamekuwa wakisingizia au kuhusisha tatizo hilo na mtandao wa shirika.
Ifuatayo ni ratiba ya mgawo wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam kutokana na kuharibika kwa transfoma kubwa katika eneo la Kipawa.
Saa 12 asubuhi – 8 mchana :-
Maeneo yatakayoathirika,
SEGEREA, KINYEREZI, BANGULO, TANDIKA YOTE, TEMEKE, MTONI MASHINE YA MAJI, YOMBO VITUKA, YOMBO BUZA, YOMBO KILAKALA, MBAGALA KILUNGULE, MAENEO YA VIWANDA YA VINGUNGUTI, KARAKATA, BANANA, KIPUNGUNI, KIVULE, KITUNDA NA MWANAGATI, AIRPORT TERMINAL ONE, AIR WING AND AIR BP
Saa 8 mchana – 4 usiku
Maeneo yatakayoathirika,
MAENEO YA CHANG'OMBE, TEMEKE MTAA WA YOMBO, KEKO TOROLI , NYERERE ROAD KUNZIA BARABARA YA KAWAWA MPAKA TAZARA NA VINGUNGUTI NA KIWALANI YOTE
Saa 4 Usiku – 12 Asubuhi
Maeneo yatakayoathirika,
SEGEREA, KINYEREZI, BANGULO, TANDIKA YOTE, TEMEKE, MTONI MASHINE YA MAJI, YOMBO VITUKA, YOMBO BUZA, YOMBO KILAKALA, MBAGALA KILUNGULE,MAENEO YA VIWANDA YA VINGUNGUTI, KARAKATA, BANANA, KIPUNGUNI, KIVULE, KITUNDA NA MWANAGATIAIRPORT TERMINAL ONE, AIR WING AND AIR BP.
Transfoma ya kituo cha kusambazia umeme cha Kipawa ya uwezo wa MVA 45 iliharibika Jumamosi saa 10:23 jioni na kusababisha baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.
Badra Masoud,
MENEJA MAWASILIANO.