Pages

May 21, 2018

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MRADI WA UUNGANISHWAJI WA UMEME WA GRIDI YA TAIFA KWA MIKOA WA LINDI NA MTWARA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa uunganishwaji umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Mradi huo sasa umeondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika kwenye mikoa hiyo ya Kusini.


NA MWANDISHI WETU, MAHUMBIKA-LINDI
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewahakikishia watanzania wote kuwa Serikali itafikisha umeme kila kona na kila kijiji.
Waziri Mkuu aliyasema hayo mara baada ya kuzindua mradi wa uunganishwaji wa umeme wa Gridi ya Taika kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye hafla iliyofanyika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.
Hata hivyo aliwataka kuwa wavumilivu kwani mipango ya serikali ambahyo ni kuhakikisha umeme unafika sio tu maeneo ya mijini bali pia kwenye vijiji vyote vya Tanzania.
“Kitendo kinachofanyika hapoa leo ni ushahjidi wa ahadi hiyo ya serikali na ninachowaomba Watanzania ni kuwa na subira kwani serikali inatekeleza ahadi ilizotoa kuhakikisha watanzania wanapata umem wa uhakika na wa bei nafuu.”
Akizungumzia uzinduzi huo ambao sasa umetoa sukuhisho la uhaba wa umeme kwenye mkoa huo wa Lindi Waziri Mkuu alitoa maagizo kwenye halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha maeneo yote nyeti ya huduma za kijamii yanafikishiwa umeme ikiwemo shule na hospitali
“Hatutarajii kuwa na eneo lenye shida ya umeme, hapa ni umeme masaa 24, na tafsiri ya serikali kuwa hapa ni umeme wa uhakika na wa kutosha ndio hii ambayo leo hii tumezindua.” Alisema.
Alisema sera ya serikali ni ya uchumi wa viwanda,na kwamba, wale watu wanaotaka kuwekeza viwanda vya Korosho, Salfa na vifaa mbalimbaki kwenye mkoa wa Lindi sasa ni wakati wao kwenda mkoani humo na kuwekeza kwani hivi sasa kuna umeme wa uhakika.
Aidha Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kuwa walizni wa miundombinu ya umeme, na kuwataka wanapoona vitendo vya watu wakihujumu mkiundombinu basi taarifa za kuwashughulikia watu hao ni vema zikatolewa kwa vyombo husika ili kuchukua hatua.
“Naomba vifaa vyote vinavyoletwa kwenye maeneo yenu, kwenye vijiji vyenu basi tuvilinde ili hatimaye tuweze kunufaika na uimarishwaji wa miundombinu ya umeme.” Aliasa Wazir Mkuu.
Kupitia mpango w REA, yaani umeme vijijini Serikali imepunguza kutoka Shilingi 380,000/= hadi shilingi 27,000/= tu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,(katikati) na viongozi wengine wa serikali wakiwemo mawaziri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kuunganishwa umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.
Waziri Mkuu Majaliwa akimpongeza Waziri Dkt. Kalemani.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (wapili kulia), akiwa na viongozi wengine, wakiimba wimbo wa taifa baada ya kufanya uzinduzi.
Waziri Mkuu Majaliwa, na viongozi wengine, akipatiwa maelezo ya ,mradi huo na mmoja wa wataalamu wa TANESCO, kwenye kituo cha Mahumbika.
Waziri Mkuu Majaliwa, akitoa hotuba yake
Waziri Mkuu Majaliwa, akitoa hotuba yake

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akitoa hotuba yake
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, akitoa maelezo ya mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, akitoa hotuba yake
Waziri Dkt. Kalemani, (katikati), akisindikizwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.

May 15, 2018

Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi TANESCO kukagua Miradi ya Umeme Arusha


 Bodi ya Wakurugenzi TANESCO imeendelea na ziara ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa kupitia mradi wa TEDAP.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi amesema miradi ya TEDAP imeboresha hali ya umeme katika Mikoa mitatu ya Dar ea Salaam,  Arusha na Kilimanjaro.

Aliongeza, Bodi imeshafanya ziara kama hiyo katika Jiji la Dar es Salaam na sasa wanamalizia katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kumepunguza tatizo la upotevu wa umeme kutokana na njia ya umeme kuwa ndefu.

Kwa upande wake  Mhandisi Emmanuel Manirabona, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Miradi alisema miradi ya  TEDAP kwa Arusha na Kilimanjaro imekamilika kwa asilimia 100 na kwa Dar es Salaam imekamilika kwa asilimia 99

Aliongeza kwa Mkoa wa Arusha mradi wa TEDAP unahusisha vituo sita ambavyo ni kituo cha Sakina, Ungalimitedi  na kill Tex.

Vingine ni Njiro B, Themi na Mount Meru.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Mhandisi Gaspar Msigwa amesema mradi  wa TEDAP umekuwa na manufaa makubwa katika kuimarisha hali ya umeme Mkoani wa Arusha.

Alisema, kabla ya kutekelezwa kwa mradi huo Mkoani Arusha  njia za umeme zilikuwa zimezidiwa sana kwani matumizi yalikuwa makubwa kuliko uwezo wa njia hizo.

Aidha,  vituo hivyo sita ambavyo vimewashwa mwezi Agosti mwaka jana, vimeonesha uwezo mkubwa wa kupunguza changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara.

" Kabla ya kukamilika kwa mradi huu Wateja walikuwa wakilalamika kupata umeme mdogo lakini kwa hivi sasa malalamiko hayo hayapo".Alisema Mhandisi Msigwa.

Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi TANESCO mbali ya kukagua mradi wa TEDAP pia ilipata fursa ya kutembelea migodi ya Mirerani na kufanya kikao na wafanyakazi wa TANESCO Mkoani Arusha .