Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka Juni 29, 2021
akizungumza na vyombo vya habari katika Ofisi za TANESCO Mikocheni
Jijini Dar es Salaam amesema kuwa, kazi ya kuimarisha mfumo wa kuuza
umeme wa malipo ya kabla (LUKU) bado inaendelea na maboresho ili
kuimarisha zaidi uwezo wa mfumo huo kwa kuuongeza mfumo mbadala
(backup).
Dkt. Mwinuka ameyasema hayo alipokutana na Waandishi wa habari kutolea
ufafanuzi jinsi TANESCO inavyojipanga kuondokana na changamoto ya
kukosekana kwa mfumo wa manunuzi ya umeme pamoja na ongezeko kubwa la
mahitaji ya umeme nchini.
Aidha, Dkt. Mwinuka ameongeza kuwa, mfumo huo wa LUKU ulianza kufanya
kazi Mei 19, 2021 mchana baada ya kutokea kwa hitlafu ya manunuzi ya
umeme Mei 17 na 18, 2021 na hivi sasa kazi ya kujenga mfumo mbadala
inaendelea.
"Hivi sasa tunaendelea na kazi ya kuhamisha taarifa kutoka kwenye mfumo
wa msingi kupeleka kwenye mfumo mbadala baada ya kuukamilisha kuujenga"
amesema Dkt. Mwinuka.
Ameongeza kuwa, katika kipindi hiki cha maboresho ya mfumo kutakuwa na
changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika manunuzi ya umeme
kutokana na majaribio katika mfumo mbadala.
Amesema iwapo wananchi wanapata changamoto ya kununua umeme kupitia
mtandao mmoja, ni vyema kutumia mtandao mwingine pamoja na huduma za
kibenki.
Pages
▼