TANESCO YATOA ELIMU YA UMEME KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI DAR.
Shirika la umeme Nchini (Tanesco) Agasti 5 na 6, 2014 imetoa
elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi Ubungo NHC na Mirambo za jijini Dar.
Meneja wa kitengo cha afya na usalama kazini Mhandisi Majige
Mabulla akitoa somo kwa wanafunzi.
|
Kaimu Meneja Mahusiano Bw. Adrian Severini akitoa elimu ya
umeme kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Mirambo.
|
Wafanya kazi wa Tanesco pamoja na wanafunzi waliopata zawadi
wakiwa katika picha ya pamoja
|
Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Mirambo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO |
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Ubungo NHC akijibu swali kutoka kwa wataalamu wa TANESCO |
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ubungo NHC wakifuatilia mafunzo. |
TANESCO YASAINI MKATABA WA KUWAUZIA UMEME SIMBA CEMENT.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO) Mhandisi, Decklan Mhaiki Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Reinhardt Swart |
TANESCO YANUFAIKA NA MAFUNZO YA TAGCO.
Idara ya mahUsiano TANESCO imenufaika na mafunzo
yaliyoandaliwa na chama cha maafisa Habari Serikalini(TAGCO),Mafunzo hayo
yametolewana Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo prof.Elisante Ole Gabriel katika ukumbi wa Karimjee, Dar es salaam.
Akitoa mafunzo hayo mwishoni mwa wiki, prof . Elisante
alisisitiza kuhusu kutoa huduma bora kwa wateja,kwani wateja ndio sababu kubwa
za kuwepo kwa taasisi za serikali,amesema wateja wanatakiwa kuhudumiwa kwa
ukarimu na Nidhamu,huku sheria na taratibu za kazi zikizingatiwa.
Sanjali na mafunzo hayo ya huduma kwa wateja,pia Maafisa uhusiano TANESCO walipata elimu
kutoka kwa mtaalamu wa Idara ya itifaki,Wizara ya Mambo ya Nje BW. Kosato Chumi
juu ya Itifaki na Protoko Serikalini.
Akizungumzia Itifaki , Bw. Kosato ameongelea taratibu zote
serikalini ,ikiwemo na swala la mavazi maofisini,ya kuwa wafanyakazi hasa
serikalini wanatakiwa kuvaa sawa sawa na taratibu zilizowekwa na serikali
katika ofisi zake,na hasa Maafisa uhusiano wanatakiwa kuzingatia zaidi uvaaji
wao hasa kwenye mazingira tofauti ya kazi zao na matukio mbalimbali ya kiofisi ,kwani wao ni
wawakilishi wa Taasisi zao.
Katika Mafunzo hayo TANESCO pia imepongezwa na Katibu mkuu
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo (WHVUM) Bi sihaka Nkinga kwa
kuonesha muitikio mkubwa wa mahudhurio
kuliko taasisi zingine za serikali zilizoshiriki.
Huu ni mwanzo tu wa Chama Hicho cha wanahabari
serikalini,ambacho kwa pamoja wamedhamiria kuimarisha utendaji bora wa shughuli
zote za Fani ya Maafisa Uhusiano na
Habari serikalini,ambapo mafunzo mbalimbali yanatarajiwa kufanyika kila robo ya
Mwaka,na hivyo kuen delea elimisha wanachama wake,TANESCO ikiwa mmoja wa
wanachama hao.
MEI MOSI 2014:
Kilio chenu ni kilio changu: Kikwete
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Mei 1, 2014, wameungana na
wafanyakazi wengine Duniani kusherehekea
sikukuu ya wafanyakazi Mei Mosi iliyofanyika
kitaifa Mkoani Dar Es Salaam. Kauli mbiu
ya mwaka huu “UTAWALA BORA UTUMIKE KUTATUA KERO ZA WAFANYAKAZI.”
Mgeni rasmi katika sherehe
hizo Mheshimiwa Raisi wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania alitoa pomgezi kwa shirikisho la wafanyakazi TUCTA kwa
kuratibu sherehe hizo na wanachi wa Dar Es Salaam kupitia kwa Mkuu wa Mkoa kwa kujitokeza
kusherehekea.
Akizungumzia kuimarika kwa Uchumi wa Taifa huku kipato cha mtu mmoja mmoja kikiwa bado cha hali
chini Mh. Raisi alisema kuimairika kwa uchumi wa Taifa kunategemea asilimia 7
ya secta
ya mawasiliano, huku sekta ya Madini, Viwanda na ujenzi vikichangia asilimia
70, sekta ya kilimo ambayo inakundi kubwa la wananchi ikiwa inakua kwa asilimia
4.3
“Sekta ya kilimo inakuwa kidogo sana ndio maana serikali
ilianzisha mkakati wa kilimo kwanza ikiwa na shabaha ya kuimarisha sekta hiyo.Pia Serikali inapambana Kushusha mfumuko wa bei akitolea mfano mwezi Mei mwaka jana ulishuka
kwa asilimia 9, mpaka kufika Mwezi mei mwaka
huu mfumuko wa bei umeshuka mpaka asilimia 6.3 alisema na aliongeza.”.
“Nyongeza ya mshahara haitakuwa na tija kama hatutapambana
na mfumko wa bei ndio maana Serikali inapambana kushusha mfumko wa bei ikiwa ni
pamoja na kuagiza bidhaa kutoka nje mfano sukari kwani viwanda vya ndani havina
uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosheleza mahitaji ya watanzania.”
Alisema migogoro sehemu za kazi hutokea pale panapokuwa
hakuna uwazi na ushirikishwaji wa wafanyakazi na wakati huo akiwataka waajiriwa kumtendea
haki mwajiri kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma na kuwataka waajiri
kuwashirikisha wafanyakazi kwenye mabaraza ya kazi. Kodi ya mapato kwa wafanyakazi ilikuwa
asilimia 18.5 mwaka 2007, imeshuka mpaka asilimia 13 kwa sasa na kuahidi
kuendelea kulishugulikia swala hilo
kwani malengo ni kufikia asilimia ya tarakimu moja.
Aliongeza madai ya wafanyakazi serikalini yatalipwa kabla ya
mwaka huu wa fedha kumalizika, uhakiki wa madeni ya walimu unaendelea, katika
halmashauri 147 halmashauri 96 ndio uhakiki wake umekamilika, na wamebaini
baadhi ya madeni si halisia ni ya kugushi. Alisema makampuni mengi hulazimika
kuajiri watu kutoka nje kwa sababu ya dhana ya watanzania hatuheshimu kazi na kujituma. “heshimuni
kazi, usicheze na kazi chezea mshahara alisema”
Aliipongeza Wizara ya kazi kwa kufuta mawakala wa ajira kwani
wamekuwa wanaajiri wafanyakazi na kuwapeleka kufanya kazi huku wakiwa waajiriwa
wao, hali hii huwakosesha wafanyakazi fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiunga
na mifuko ya hifadhi ya jamii, likizo, matibabu na kukatwa mishahara yao huku akikiita kitendo hiki kama
dhuluma, alisema malengo ya mawakala hawa ilikuwa watumike kama daraja la kuwaunganisha
watafuta kazi na waajiri .
Mh. Raisi pia alitoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa
mwaka huku mfanyakazi bora kitaifa
kutoka Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini TANESCO Bw. Joel Peter Kibonge akiwa
miongoni mwa wafanyakazi bora
32waliopewa tuzo na Mh. Raisi.
Mgeni rasmi alimalizia kwa kushukuru kupewa nafasi na kuahidi kutatua changamoto
zinazo wakabili wafanya kazi “kilio
chenu ni kilio changu alisema” na kuahidi maslahi mazuri kwa wafanyakazi.
TANESCO YAWAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2014
Shirika la umeme nchini TANESCO Mei 1, 2014 limefanya hafla fupi
ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa
matawi na idara pamoja na mfanyakazi
bora kitaifa mwaka 2014 Bw. Joel Peter Kibonge ambaye ni fundi mchundo kutoka kituo cha uzalishaji
umeme Loliondo Mkoani Arusha. Sherehe
hizo zilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Shirika.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Kaimu mkurugenzi wa TANESCO
Mhandisi Decklan Mhaiki aliwapongeza
waliochaguliwa kuwa wafanyakazi bora na kusema shirika limeona umuhimu wa
kuwapongeza na kuboresha zawadi kutoka
radio na kuwa TV za nchi 32.
Alisema zawadi hizo ziwe chachu kwa wafanyakazi kufanya kazi
kwa bidii, ufanisi, na ubunifu ili
kuweza kujenga TANESCO yeneye ufanisi. Alimpongeza mshindi wa kitaifa na kusema
hakupatikana kwa bahati balli vigezo vilizingatiwa na yeye kuwa mshindi.
Kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa TUICO TANESCO Makao Makuu Bw. Ally Mkama alisema
mfanyakazi bora wa mwaka ameweza kupata zawadi ya TV nchi 32, cheti, hundi ya
pesa za kitanzania shilingi milioni 3 na pia atachagua Nchi yoyote Duniani
atakayopenda kwenda kutembea pamoja na mwenza wake kwa muda wa siku saba.
Mshindi kitaifa Bw. Kibonge alisema anafurahia kuwa
mfanyakazi bora na kuwataka wafanyakazi
wengine kufanya kazi kwa bidii na hari mpya pia kuongeza mshikamano katika
utendaji.Pia alitumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa shirika na wafanyakazi
kwa ujumla.
WATEJA MITA ZA KAWAIDA KULIPA BILI KWA NJIA YA MTANDAO KIBENKI
Mei 2, 2014 Shirika la Umeme nchini TANESCO limezindua
huduma ya malipo ya bili kwa njia ya mtandao na benki kwa wateja wa Kinondoni kusini
wanaotumia mita za kawaida.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema lengo la kuanza kwa
huduma hii ni kuwawezesha wateja wanaotumia mita za kawaida kuweza kulipa bili
zao pasipo kupata usumbufu wa kutembea umbali mrefu kwenda kwenye ofisi za
TANESCO na kupanga foleni ili kulipia bili zao.
“Katika kuboresha
huduma zake kwa wateja shirika lipo kwenye mkakati wa kuanzisha mawasiliano na
mteja kwa njia ya SMS inapo tokea tatizo
sehemu husika, akitolea mfano kukatika kwa umeme ama panapokuwa na matengenezo
ya kuboresha miundo mbinu”.
Kwa sasa wateja waTANESCO
Kinondoni Kusini wanaotumia mita
za kawaida wanaweza kulipa Ankara kupitia simu zao za mkononi kwenye mitandao
ya Tigo, Vodacom na Airtel pia kupitia Mashine za Maxcom na Selcom zitatoa huduma ya kulipia Ankara kama
zinavyoweza kuuza umeme kwa wenye mita za LUKU alisema.
Nae Meneja Mwandamizi kanda ya Dar Es Salaam na Pwani
Mhandisi Mahende Mugaya alisema mkoa wa
kinondoni kusini umefanikiwa kupunguza deni kwa kukusanya mapato, “ huduma hii
mpya itakuwa na faida kwa wateja na TANESCO kwani itamuwezesha mteja kulipa bili mahali
popote alipo na kwa urahisi. Pia itaokoa muda na ni njia salama kabisa ya
malipo alisema.”
Kwa upande wake Kaimu Naibu Mtendaji usambazaji na huduma
kwa wateja Mhandisi Nicholaus Kamoleka alisema utumiaji wa malipo kwa njia ya mtandao
ni mpya kwa TANESCO , pia ni maagizo kutoka serikalini. “ Mwaka jana Shirika
lilivuka malengo kwa kuwaudumia wateja
laki moja na elfu arobaini na tatu alisema.”
WIZARA NISHATI YAWAKABIDHI WAHANDISI ZAWADI
Wizara ya nishati na madini imewazadia mafundi wa TANESCO
jumla ya shilingi za kitanzania milioni 48.8 kutokana na kufanya kazi usiku na
mchana kurejesha umeme katika kituo cha kupooza umeme cha Ubungo Msongo wa kilovoti 33.
Kituo hicho kilipata ajali ya kuungua moto Januari 11, 2014
na kuathiri upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Magomeni, Ubungo, Ilala na
maeneo ya chuo Kikuu.
Akikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Waziri wa Nishati na
Madini Naibu Kamishina Bw. Innocent Luhoga alitoa sifa kwa wahandisi wa TANESCO
kwa kufanya kazi kwa kujituma, akitolea mfano miundo mbinu inavyoathirika
kipindi cha mvua, waandisi hujitahidi
kurejesha huduma kwa wakati.
Pia alitoa salamu kutoka kwa katibu mkuu wa wizara “katibu
mkuu wa nishati na madini anawashukuru wafanyakazi kwa yote” Wizara inatambua
mnavyo fanya kazi katika mazingira magumu licha ya wakati mwingine watu
kuwasema vibaya ama magazeti kuwaandika
vibaya alisema.
Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia. |