Pages

December 2, 2010

Kishoka mwingine ahukumiwa miaka mitatu jela

Kishoka Mansoor mwenye T-shirt ya TANESCO akiwa na mwenzake Jose Kifman

Vishoka hao wakiteremshwa na polisi

Kishoka maarufu Mansoor Ibrahim (pichani) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli za TANESCO huku akiwa si mfanyakazi wa TANESCO mbele ya hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Kisutu Mhe. Mwaseba.
Kishoka huyo alikamatwa mwezi machi mwaka huu maeneo ya Tabata Kilungule akitaka kumrubuni mteja wa TANESCO Bw. Seleman Njonanje. Alifunguliwa jalada kituo cha Polisi Kati na hatimaye mahakamani kwa kesi namba CC.236/09.
Kishoka huyo Bw. Mansoor akiwa na kitambulisho chenye jina la Mwijage na sare za Shirika alimghilibu mteja kuwa mita yake ni mbovu na anakwende kuibadilisha na akapatiwa Sh. 500,000/-.

No comments:

Post a Comment