Pages

December 8, 2010

NGELEJA ATEMBELEA MITAMBO YA KUFUA UMEME

Waziri wa Nishati na Madini, Mh. William Ngeleja ametembelea mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo jijini Dar es Salaam kujionea hali halisi ya ufuaji wa umeme nchini.

Katika ziara yake hiyo iliyohusisha maafisa wa juu wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, iliambatana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

Mitambo aliyotembelea ni pamoja na Songas wenye uwezo wa kuzalisha 180MW ambapo kwa sasa unaingiza wastani wa 132MW kwenye gridi ya taifa, IPTL yenye uwezo wa kuzalisha 100MW leo umefikia 70MW na Mtambo wa Tegeta wenye uwezo wa kufua 45MW ambazo zote zinafuliwa kwa sasa na kuingia kwenye gridi ya taifa.

Waziri alipotembelea kituo kikuu cha kudhibiti gridi ya taifa kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam, alipata maelezo kuwa asubuhi ya leo hakukuwa na mgawo wa umeme sehemu zozote nchi nzima mbali na makatizo mengine ya kawaida.Hii inatokana na kuongezeka kwa maji kwenye bwawa la maji la Kihansi.

Aidha waziri alipotembelea mtambo wa Songas aliahidiwa kurejeshwa kwa mtambo mwingine wenye uwezo wa kuzalisha 32MW uliokuwa kwenye matengezo kabla ya mwisho wa wiki hii.

Mh. William Ngeleja akiwa na Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Mhandisi William Mhando wakiingia kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Songas

Meneja Mtambo wa Songas, Bw. Robert Kofsky akitoa maelezo  kuhusu uzalishaji wa kituo hicho

Meneja Mtambo wa Songas akimuonesha Mh. Ngeleja mtambo uliokuwa kwenye matengenezo unaotarajiwa kuanza kufanya kazi mwishoni mwa wiki hii

Mh. Ngeleja na maafisa wengine wa TANESCO wakibadilishana mawazo kabla ya  kuelekea kwenye mitambo ya Songas
Mh. Ngeleja akiongea na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo

Mkurugenzi Mtengaji wa TANESCO, Mh. William Mhando akitoa maelezo kuhusu kituo cha kudhibiti gridi ya Taifa kilichopo Ubungo

Mh. Ngeleja(wa pili kulia) akipotembelea ndani ya kituo cha kudhibiti gridi cha Ubungo kujionea teknolojia mpya ya digitali inayotumika katika kituo hicho kwa sasa

Mh. Ngeleja(katikati) alipokuwa anatembelea mitambo ya kufua umeme wa mafuta cha IPTL

Mh. Ngeleja akioneshwa shughuli ya upakuaji wa mafuta katika kituo cha kufua umeme cha IPTL

Mh. Ngeleja alipotembelea mitambo ya kufua umeme cha Tegeta akiongozwa na Meneja wa kituo hicho Mhandisi  Mohammed Kissiwa (aliyeshika bahasha)

Meneja Mkuu wa TEKNOHAMA TANESCO, Bi. Salome Nkondola akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu tatizo la LUKU katika vituo mbalimbali vya kuuza LUKU nchini.

1 comment:

  1. Wakazi wa viwanja vya mradi Bunju BDecember 23, 2010 at 5:27 AM

    Wakazi wa viwanja vya mradi Bunju B said...

    Bunju B viwanja vya mradi tuna shida ya umeme, tuelezeni tufanye nini zaidi ya maombi ya umeme ili tuwe na mwanga usiku.
    Hela zakulipia gharama tunazo, hela za luku tunazo, sasa kazi kwenu mtuongeze kwenye "customer base" yenu, ambayo ndio msingi wa biashara yenu.
    Kazi kwenu TANESCO.

    ReplyDelete