Pages

March 5, 2012

Shirika lawapongeza mafundi wa kikosi maalumu cha karabati umeme Dar.



Meneja Uhusiano, Bi. Badra Masoud, akisakata rumba 
pamoja na mafundi wa KAUDA.
Baada ya Kikosi maalumu cha kukarabati umeme Dar es salaam(KAUDA), kumaliza kazi ya kufikisha umeme kwa muda mfupi, wa siku kumi na nne, Shirika lawapongeza kwa tafrija fupi iliyofanyika katika viunga vya Chuo cha TANESCO, Masaki.


Kufuatia janga la mafuriko lililoyakumba baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es salaam miezi miwili iliyopita na Serikali kuamua kuwapatia waathirika maeneo salama ya makazi katika kijiji cha Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Tarehe 13 Januari, Mh. Rais Jakaya Kikwete, aliomba Taasisi zote zinazotoa huduma muhimu kama Maji, Barabara na Umeme, kutoa ahadi ya lini watafikisha huduma hizo haraka. Meneja Mahusiano wa Tanesco,Bi. Badra Masoud ambaye alimwakilisha,Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mwandisi William Mhando, kwakutambua umuhimu wa huduma ya umeme kwa waathirika, , alitoa ahadi ya siki 14 kumaliza kuweka miundombinu ya umeme.  Kikosi maalumu cha kukarabati umeme Dar es Salaam (KAUDA) walikabidhiwa jukumu ilo.

Hatimaye tarehe 05, Feb tumeweza kufikisha umeme kwenye viunga vyote vya makazi mapya ya Mabwepande. Meneja Mahusiano, Bi. Badra Masoud ametembelea maeneo ya ujenzi wa mradi na kushuhudia ujenzi umekwisha na taa chache zilizowekwa kwenye nguzo.
Ndipo Uongozi wa Shirika wakaamua kuwapongeza KAUDA kuonyesha kutambua kazi ngumu waliyoitekeleza , lakini  pia kupata nafasi ya kusikia toka kwao.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando, 
akipokea risala ya mafundi wa KAUDA

Mafundi wa KAUDA wakipata chakula katika tafrija 
ya kuwapongeza

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, William Mhando
akipata chakula cha jioni, pamoja na mafundi wa KAUDA.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,. Mhandisi, William Mhando
akiwapongeza mafundi wa KAUDA kwa kupita katika meza zao

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, William Mhando
 akiwa katika picha ya pamoja na mafundi wa KAUDA.

No comments:

Post a Comment