Pages

October 2, 2012




TANESCO Mpya Iweje

Wapendwa wateja wa TANESCO na wananchi wote kwa ujumla, Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ni mali ya Umma kwa kuwa linamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100. Hivyo TANESCO ni mali ya watanzania.
Kwa kulitambua hilo, Uongozi wa Shirika umeanzisha mchakato wa kufanya mabadiliko ya KIMUUNDO na KIUTENDAJI kwa Shirika, ili kuhakikisha kuwa TANESCO inatoa huduma zake kwa ufanisi zaidi na kwa matakwa ya wananchi na wateja wake.
Tunakaribisha maoni, ushauri, mapendekezo kutoka kwa wananchi, wateja wote wenye mapenzi mema na maendeleo ya TANESCO na nchi yetu kwa ujumla.
Tafadhali tutambue kuwa nia ya mchakato huu ni kujenga, hivyo tutoe maoni kwa nia njema.
Unaweza pia kutoa maoni yako kwa kupitia
tanesco.iweje@tanesco.co.tz,
communications.manager@tanesco.co.tz au facebook kwa kutafuta neno
‘tanesco iweje’au kwa kupiga simu namba +255222451185

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.

4 comments:

  1. TANESCO mkitaka Shirika liwesafi msisite kuwashughulikia wafanyakazi wanaowaangusha. Wapo wafanyakazi ambao kweli ni waadilifu, lakini wengine si waadilifu. Kama mlivyosema TANESCO ni mali yetu ni kweli kabisa. Hii itakuwa kazi kubwa na nzuri. Big up TANESCO kwa mchakato huu. Hakikisheni mnachukua maoni kama ya Katiba Mpya.

    ReplyDelete
  2. Maoni yangu yako upande wa kununua umeme kwa njia ya mobile.unaweza ukanunua luku ukakatwa pesa toka kwenye akaunti yako lakini usipewe luku zako.Nasema hivyo kwa sababu hilo limenikuta mimi wiki iliyopita nilipokwenda benki hisika niliambiwa sisi hatuhusiki na hilo anayehusika na hilo ni tanesco aliyechukua pesa ya mteja wetu kwenye akaunti yake bila kumpa huduma aliyoistahili.Nilifika ofisi ya tanesco nikaambiwa tena wao hawahusiki na hilo,nikawauliza kwani system yenu haionyeshi rekodi za ununuaji wa umeme wa mita yangu? Nikajibiwa hilo hadi makao makuu dar es salaam.Swali ninalowauliza mbona ninaponunua umeme kwa mobile nikakatwa serivice charge mbona nikienda tanesco huwa sirudii kukatwa kwa sababu system tayari imekwishatambua nimekwishakatwa service charge kupitia mobile,Hivyo kwanini tusiwe tunapewa rekodi nzima ya lini na wapi mita yako imenunua luku kama unavyopewa bank statment?,mbona nikitoa pesa kwa atm siku nikienda benki nikiomba mnyambulisho wangu napewa.

    ReplyDelete
  3. Menejimenti na watoa huduma wa TANESCO;

    Naanza kwa kutoa pongezi na shukrani nyingi sana kwenu kutokana na utendaji wenu unaohanikizwa na changamoto lukuki.

    Kwa hiyo acheni changamoto hizo ziendelea kuwa sehemu ya utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku badala ya kikwazo.

    TANESCO mpya iweje ni swali fupi sana kwa mtazamo wa haraka,lakini unapochungulia nyuma ya pazia linaonekana kuwa na urefu usio na kipimo kamili.

    Tukumbuke kuwa hapa tunafuta suluhisho la kudumu la changamoto zinazolikalibili shirika hili muhimu katika uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme.

    Mimi nakubaliana na wazo hili la kuwashirikisha wadau katika kutoa mawazo yao ambayo nahisi yatakuwa na ladha ya kibiashara zaidi kuliko kitaaluma.

    Madokezo ya kitaaluma katika tasnia ya uzalishaji umeme na usambazaji wake ndiyo yatayoweza kuzaa TANESCO mpya yenye muonekano mpya (chupa mpya na mvinyo mpya na siyo chupa mpya na mvinyo wa kizamani) na siyo TANESCO mpya yenye muonekano wa zama za ujima.

    TANESCO kupitia wizara ya Nishati na Madini iwatafute wanazuoni mahiri na makini kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kwa pamoja wakutane mezani kwa ajili kufanya tafiti za kina kirefu.

    Nadhani TANESCO inaweza kugawanywa katika maeneo kadhaa, na hapa nataja machache:

    1.Miundombinu ya kuzalisha nishati ya umeme
    2 Kusambaza nishati ya umeme
    3.Mauzo ya umeme.

    Wenu kwa staha;

    Ray E.Njau
    Mdau wa TANESCO
    Mkoa wa Ilala
    Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  4. nyinyi ni wazembe tu mtu akiomba kuwekewa umeme nenda mkamuwekee sio kusubiri mpaka aje ofisini kubembeleza kama vile mnampa bure huo umeme

    ReplyDelete