Pages

June 19, 2013

TAHADHARI WIZI WA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA


SHIRIKA LA UMEME TANZANIA- TANESCO

TAHADHARI WIZI WA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA

Kwa masikitiko makubwa, Shirika la Umeme Tanzania - TANESCO linasikitishwa na vitendo vinavyoendelea vya kuhujumu miundombinu ya Shirika ikiwepo kuibiwa nyaya za umeme huko Arusha mwezi mmoja uliopita, kuibiwa kwa vyuma vya nguzo huko Morogoro na siku ya Jumapili Juni 16, 2013 kuibiwa mafuta pamoja na winding za transfoma iliyopo Mbezi Kibamba kwa Tendwa jijini Dar es Salaam. Wizi huu unatokea wakati Shirika linajitahidi kuboresha huduma zake kote nchini.

 Kutokana na wizi huo, wateja zaidi ya 150 waliathirika kwa kukosa umeme tangu Jumapili hadi jana jioni Juni 17, 2013 ambapo Shirika ilibidi litafute na kufunga Transfoma nyingine ambayo ilikuwa imepangwa itumike kusambaza umeme kwa wateja wengine ambao hawajawahi kupata huduma ya umeme kabisa.

Uongozi wa Shirika unasikitika kwa vitendo hivi na unawaomba wananchi wote kutoa taarifa Polisi au Ofisi zozote za TANESCO zilizopo karibu nao wanapoona watu wanaowatilia shaka kutaka au kuhujumu miundombinu ya Shirika.

Au wasiliana nasi, Kituo cha Miito simu namba 2194400 au 0786985100 

 "Tuilinde Miundombinu ya TANESCO kwa maendeleo yetu na Taifa kwa ujumla"


 Imetolewa na:

                          OFISI YA UHUSIANO,
                          TANESCO - MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment