Pages

June 28, 2013

TANGAZO

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI TANGAZO

 Mkurugenzi wa TANESCO anawatangazia ndugu na jamaa wa Marehemu waliozikwa kwenye Makaburi yaliyopo ndani ya eneo la mradi wa upanuzi wa njia za umeme Kata ya Manzese, Mtaa wa Midizini na Kata ya Ubungo Mtaa wa Ubungo Kisiwani kwamba anakusudia kuhamisha Makaburi hayo 250 ili shughuli ya upanuzi wa njia ya umeme iweze kuanza.

 Kwa mujibu wa Sheria za mitaa (Mamlaka za Miji) ya mwaka 1982, kanuni ya mwaka 2008 namba 46(c) Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itasimamia zoezi hili kwa kutumia wataalam wake.

Taarifa inatolewa kuwa watu wote wenye ndugu au jamaa waliozikwa kwenye eneo hilo wafike Ofisi za Afisa Mtendaji wa Kata za Manzese na Ubungo kujiandikisha wakiwa na barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Mtaa anaoishi kabla ya tarehe 25/07/2013.

 Makaburi hayo yatahamishiwa kwenye Makaburi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yaliyoko Tegeta Kata ya Kunduchi baada ya taratibu zote kukamilika.

                                                              (Imesainiwa na)
                                                     Eng. Mussa Natty Mkurugenzi wa Manispaa
                                                   HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

No comments:

Post a Comment