Pages

August 15, 2013

KATIZO LA UMEME

                                         SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

KATIZO LA UMEME MIKOA YA  KILIMANJARO NA ARUSHA

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wote wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI 17/08/2013 na JUMAPILI 18/08/2013 kuanzia Saa 02:00 Asubuhi hadi Saa 10:00 Jioni.  SABABU ni   kuzimwa kwa laini kubwa za umeme za (132 Kv) Kiyungi –
Njiro, (66 Kv) Kiyungi- Njiro, pamoja na (33 Kv) K40 ili kupisha ujenzi wa njia ya mfumo wa mawasiliano katika kituo kipya cha kupozea umeme cha KIA na kubadilisha nguzo kwenye laini ya umeme ya USA.
MAENEO YATAKAYO ATHIRIKA:
WILAYA YA HAI, WILAYA YA SIHA YOTE, MERERANI PAMOJA NA BAADHI YA MAENEO YA KIN’GORI,      UZUNGUNI, PAMOJA NA KIWANDA CHA TANZANIA BREWERIES MKOA WA ARUSHA
                                                        
‘‘usiguse wala kusogelea waya uliokatika au kuanguka chini, toa taarifa kwenye ofisi ya TANESCO    kupitia namba 0272755007, 0272755008, na 0272754035
SHIRIKA LINAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAO JITOKEZA
IMETOLEWA NA:  OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment