Pages

September 23, 2013

FURSA PEKEE

LIPA DENI LA UMEME USAMEHEWE RIBA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wenye madeni ya umeme kuwa linatoa msamaha wa riba kwa kipindi cha miezi sita (6) kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2013 hadi tarehe 31 Machi, 2014.
Katika kipindi hicho wateja wenye madeni wataruhusiwa kulipa madeni yao bila riba kwa sharti la kumaliza kulipa deni lote katika kipindi cha miezi sita.
Ili unufaike na fursa hii tafadhali fika kwenye ofisi ya TANESCO ya Mkoa au Wilaya iliyo karibu nawe, na uingie mkataba ya kulipa deni ndani ya miezi sita bila riba.
Msamaha wa riba utatolewa kwa mteja yeyote wa TANESCO mwenye madeni ya muda mrefu.
Usiikose fursa hii maalum na ya pekee. Lipa deni lako sasa, ufurahie huduma bora za umeme.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI - TANESCO

No comments:

Post a Comment