Pages

September 19, 2013

KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANI NA KILIMANJARO



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Wilaya ya Mkuranga na Same kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya  Jumamosi Septemba 21, 2013 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni. 

Sababu ni: Kufanya matengenezo kwenye laini ya Msongo    wa 33 KV Maweni na Mkuranga na Kubadilisha nguzo zilizo oza katika laini ya msongo wa kilovolt 33 ya Makanya-SAME

Maeneo yatakayoathirika ni :- 
Wilaya ya MKURANGA ni: Kiwanda cha Maweni, maeneo yote ya Viwandani pamoja na mji wa Kisemvule na mkuranga mjini

Wilaya ya SAME ni: : Makanya, Vudee, Chome, Suji, Tahe Saweni pamoja na
                                           Hedaru


Tafadhali usishike, usikanyage wala kusogelea nyaya za umeme zilizolala chini, ijulishe TANESCO mara moja kwa simu na: Mkoa wa Pwani:0657 108782 au Call centre namba 2194400 au 0768 985 100
SAME: 0272755007, 0272755008, na 0682771310.0765397925
         


.Uongozi unasikitika kwa  usumbufu wowote utakaojitokeza.

IMETOLEWA NA:   OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.
 

No comments:

Post a Comment