Pages

September 23, 2013

TAARIFA FUPI YA KISHOKA ALIYEKAMATWA MKOA WA TEMEKE



Siku ya Jumanne tarehe 17-09-2013 Mkoa wa Temeke ulimkamata KISHOKA  aliyejitambulisha kwa jina la Benard Kilembe mkazi wa Yombo Vituka. Kishoka huyu alieleza kuwa aliwahi kuwa mfanyakazi wa muda maalum Tanesco-Mbeya  miaka ya 1995-1997. 
 
Baada ya kupekuliwa nyumbani kwake, alikutwa na nyaraka mbalimbali za shirika kinyume na taratibu, sare ya Ijumaa(T shirt)  na Shati la Sare za mafundi, Rakili mali za Shirika (seal), vipande vya nyaya 50mm na 25mm,kitambulisho cha aliye kwenye mafunzo  na  na pamoja na hayo alikuwa amejiunganishia umeme kinyume cha taratibu.
Kishoka huyu bado yupo chini ya ulinzi kwenye kituo cha polisi Chang’ombe akiisaidia polisi na uchunguzi zaidi.

 


 Akiwa chini ya ulinzi 

Daftari la wateja anaowatembelea

Kitambulisho anachotumia kufanya shuguli zake



No comments:

Post a Comment