Pages

October 17, 2013

KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Pwani kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI tarehe 19.10.2013 kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi 10 Jioni.  Sababu ni kufunga nyaya kwenye laini mpya iendayo Msanga - Mwanelumango kwenye njia ya umeme ya msongo wa 33kV.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:-
Mwisho wa Lami, Pugu, Majohe, Chanika, Buyuni, Kipawa mpya na Kisarawe.
Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo: 0657 108782 au Kituo cha Kupokelea miito ya simu 2194400 au 0768 985 100
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na:- OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.
                  
                         

No comments:

Post a Comment