Pages

October 9, 2013

PWANI

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Bagamoyo kuwa hakuna umeme katika sehemu kubwa ya Mji wa Bagamoyo kuanzia JUMAPILI tarehe 06/10/2013 muda wa mchana hadi sasa kutokana na transfoma kubwa la MVA 2.5 la msongo wa kilovoti 33/11 lililopo Mwanamakuka kupata hitilafu. Mafundi bado wanaendelea na kazi ili kurejesha huduma ya umeme katika hali ya kawaida.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.              
                           

No comments:

Post a Comment