Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu
wateja wake wa Mkoa wa Ilala na Temeke kuwa
kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-
MKOA WA ILALA:-
TAREHE:
Jumapili, 02 Machi, 2014
MUDA: Saa 03:00 asubuhi hadi12:00
jioni .
SABABU: Kufanya Matengenezo
Kwenye Vifaa vya Kudhibiti Umeme Kwenye Njia za
Umeme za Msongo Mkubwa
wa ‘33kV Breakers’ za Industrial na UB0
Feeders.
MAENEO
YATAKAYOATHIRIKA:
Julius Nyerere International Airport, TAZARA,
baadhi ya Viwanda vilivyoko Barabara ya
Nyerere na baadhi ya maeneo yaliyoko kandokando ya Barabara ya Mandela. Maeneo mengine ni; Tabata,
Liwiti, Kimanga, Kisukuru, Makoka, Tabata Kisiwani, Tabata Shule, Bima, Aroma na
maeneo yanayozunguka.
MKOA WA TEMEKE:-
TAREHE: Jumapili 02/03/ 2014
MUDA: 03:00
Asubuhi – 12:00 jioni
SABABU: Kukata miti kwenye laini ya umeme.
MAENEO
YATAKAYOATHIRIKA:
Maeneo
yote ya Navy, Mwalimu Nyerere, Ferry, Mikadi beach, Magogoni, Tungi na maeneo
yanayozunguka.
Tafadhali usishike wala kukaribia waya wa
umeme uliokatika, toa taarifa kupitia namba zifuatazo: Dawati la dharura Mkoa
wa Ilala 0715768586, 0715768587, 0684001066, 0680001068. Dawati
la dharura Mkoa wa Temeke 0222138352, 0732 997361, 0712 052720, au Kituo cha
miito ya simu 022 2194400 /0768 985 100
Uongozi unasikitika Kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewana: OFISI
YA UHUSIANO,
TANESCO –
MAKAO MAKUU.