Pages

February 28, 2014

KATIZO LA UMEME – MKOA WA ILALA NA TEMEKE



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala  na Temeke kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

MKOA WA ILALA:-

TAREHE:   Jumapili, 02 Machi, 2014

MUDA:       Saa 03:00 asubuhi hadi12:00 jioni          .  
                                               
SABABU:  Kufanya Matengenezo Kwenye Vifaa vya Kudhibiti Umeme Kwenye Njia za
        Umeme za Msongo Mkubwa wa ‘33kV Breakers’ za Industrial na UB0
        Feeders.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Julius Nyerere International Airport, TAZARA, baadhi ya Viwanda vilivyoko Barabara ya  Nyerere na baadhi ya maeneo yaliyoko kandokando ya  Barabara ya Mandela. Maeneo mengine ni; Tabata, Liwiti, Kimanga, Kisukuru, Makoka, Tabata Kisiwani, Tabata Shule, Bima, Aroma na maeneo yanayozunguka.

MKOA WA TEMEKE:-

TAREHE:       Jumapili  02/03/ 2014 

MUDA:            03:00 Asubuhi – 12:00 jioni

SABABU:       Kukata miti kwenye laini ya umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Maeneo yote ya Navy, Mwalimu Nyerere, Ferry, Mikadi beach, Magogoni, Tungi na maeneo yanayozunguka.

Tafadhali usishike wala kukaribia waya wa umeme uliokatika, toa taarifa kupitia namba zifuatazo: Dawati la dharura Mkoa wa Ilala 0715768586, 0715768587, 0684001066, 0680001068.   Dawati la dharura Mkoa wa Temeke 0222138352, 0732 997361, 0712 052720, au Kituo cha miito ya simu 022 2194400 /0768 985 100

Uongozi unasikitika Kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.



Imetolewana:             OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment