Pages

June 2, 2015

TAARIFA

KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA KINONDONI KUSINI.

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)linawataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa kuna hitilafu ya umeme imetokea kwenye kituo cha kupooza na Kusambaza Umeme cha Ubungo upande wa msongo wa kilovolti 33 na hivyo kusababisha maeneo ya Manzese,Tandale,Kigogo,Sinza, Mabibo, Ubungo, Mandela Road, Makoka, Msewe, Makongo, Changanyikeni, Kimara, Mbezi Luis, Makabe, Goba Juu, Kibamba na UDSM kukosa umeme.

Unatarajia kurudi saa 2 usiku baaada ya kubadili kifaa kilichoharibika.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment