Pages

February 29, 2016

UFAFANUZI JUU YA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU OMBI LA TANESCO KUSHUSHA BEI YA UMEME



UFAFANUZI JUU YA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO
VYA HABARI KUHUSU OMBI LA TANESCO KUSHUSHA BEI YA UMEME

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewasilisha ombi la kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1.1 kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) pamoja na kuondoa kabisa gharama ya maombi ya awali kwa wateja wapya (gharama za Fomu) ya Shilingi 5,000 na gharama za huduma (service charge) ya Shilingi 5,520 kwa mwezi kwa wateja wote wa majumbani.

Maombi hayo yamewasilishwa baada ya TANESCO kufanya tathmini ya kina ya kimahesabu pamoja na kubuni namna ambayo wateja wake wanaweza kupata ahueni ya gharama kwa kuzingatia mazingira ya sasa.

Hata hivyo baadhi ya vyombo vya habari vimepotosha ukweli huo hivyo TANESCO inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:-
Mosi, Kwa mujibu wa sheria, TANESCO inapotaka kubadilisha bei za umeme, iwe kushusha au kupandisha ni lazima iwasilishe maombi hayo EWURA kwa kuwa ndiyo mwenye mamlaka ya kisheria ya kubadilisha bei za umeme.

Pili, TANESCO huwasilisha maombi yake pamoja na takwimu halisi zinazoshawishi mantiki ya kubadilishwa kwa bei hizo na kwa maombi yaliyowasilishwa EWURA Februari 24, 2016 ndivyo TANESCO ilivyofanya.

Tatu, Baadhi ya mambo muhimu yanayoendana na mazingira ya sasa ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme wa gesi tofauti na ilivyokuwa hapo kabla na pia kuongezeka kwa ujazo wa maji katika mabwawa hasa Mtera.

Nne, japokuwa kiasi cha madeni kilichotajwa na vyombo vya habari sio sahihi, madeni hayo yamezingatiwa kikamilifu katika mapendekezo haya ya kushusha bei, hivyo si kweli kwamba kwa kushusha huko bei TANESCO itafilisika.

Aidha, kusema kwamba Serikali inailazimisha TANESCO kushusha bei ya umeme na kwamba kwa kufanya hivyo Shirika litafilisika sio sahihi hata kidogo kwani tathmini ya kitaalamu imefanyika na pia kwa mujibu wa sheria EWURA itafanya tathmini yake kabla ya kuidhinisha bei mpya.

Ieleweke kwamba Serikali ya awamu ya Tano imeshatoa fedha nyingi za kusaidia miradi ya umeme zikiwepo zaidi ya Shilingi Bilioni 100 zilizotolewa hivi karibuni kwa maelekezo ya Mh. Rais kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa Mradi mkubwa wa Kinyerezi II unaotekelezwa na Kampuni ya SUMITOMO ya Japan.

Pia Serikali imeendelea kulipa madeni ya umeme ya taasisi zake na hadi sasa sehemu kubwa ya madeni ya taasisi za Serikali yamelipwa.

Hivyo, TANESCO inaishukuru Serikali kwa jitihada kubwa inazozifanya katika kushughulikia changamoto za umeme nchini.

Imetolewa na:  Ofisi ya Uhusiano,
                         TANESCO Makao Makuu.

February 25, 2016

EMPLOYMENT OPPORTUNITY INTERNAL AND EXTERNAL ADVERTISEMENT



 

The Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is focusing on increasing the outreach and service quality of its Energy products for Tanzanian people.  Next to its current passion as a leading provider of electricity, is to be more efficient customer focused utility for Tanzania and beyond. The Company has the largest electricity generation, transmission and distribution network in Tanzania. In order to reach its goals, the Company will, in the coming years invest heavily in its generation, transmission and distribution network, its business systems and human capital. TANESCO now invites applicants who are self-motivated, honest, hardworking and committed individuals to fill top management positions in the Company. Women are encouraged to apply.

Specific attributes for the Position to be filled:

The required candidate must:

v  Demonstrate impeccable performance track record;
v  Demonstrate highest degree of integrity;
v  Possess good communication and interpersonal skills;
v  Possess leadership, project management, problem solving, negotiation, research and analytical skills.
v  Be capable of delivering excellent results while working under pressure with tight deadlines;
v  Possess knowledge and competency in Information and Communication Technology (ICT) application.


Position:            CHIEF LEGAL COUNSEL & COMPANY SECRETARY
Reporting to:     Managing  Director
Division:            Company Secretariat


JOB PURPOSE

Responsible for the efficient administration of the company particularly with regard to compliance
with statutory and regulatory requirements and ensuring that decisions of the Board of Directors
are implemented.

PRINCIPAL ACCOUNTABILITIES:

1.    Perform a strategic role to the executive management and the board as a secretary to all meetings and ensure proper and accurate records of the proceedings are kept.

2.    Manage and supervise the secretariat function to ensure that it contributes to the strategic effectiveness and operational efficiency of the organization and that it achieves its objectives as planned.

3.    Manage the secretariat functions (litigation, contracts, legal and regulatory compliance) and processes.

4.    Monitor changes in relevant legislations and the regulatory environment, and take appropriate actions to communicate and adopt them in TANESCO to ensure compliance.

5.    Promote proactive and constructive management of secretariat business unit by developing appropriate strategic objectives for secretarial, contract and legal sections for the purpose of supporting all business units of the Company.

6.    Assist in execution of contracts on behalf of the Company by contributing effectively in the business processes redesign and policies review.

7.    Custodian of the Company Seal and Legal documents.

8.    Manage, develop and ensure proper utilization of resources (human capital, financial and other Company assets) within the department in order to support Corporate Business sustainability.


MINIMUM EDUCATION AND EXPERIENCE:

·         Bachelor Degree in Law (LLB)
·         Master’s Degree in Law/Business Administration
·         Advocate of the High Court of Tanzania.
·         8 years working experience (3 years in Senior Managerial Position)

Position:            SENIOR MANAGER PROCUREMENT
Reporting to:     Managing  Director
Division:             Procurement

JOB PURPOSE:

Lead and manage the implementation of the approved Company’s procurement and disposal plans.

PRINCIPAL ACCOUNTABILITIES:

1.    Prepare and manage the annual procurement plan of the Company taking into account the needs and resources.

2.    Manage and facilitate the entire procurement process as well as and disposal by tender activities of the Company.

3.    Act as a secretary to the Tender Board, and ensure proper functioning of the Tender Board and coordinate the implementation of its decisions.

4.    Keep records on all procurement and disposal by tender processes including maintaining a register of all contracts awarded.

5.    Manage key supplier relationship to deliver performance in cost saving and quality including technical input for negotiation on strategically significant contracts.

6.    Manage and maintain good business relationship with Service providers, contractors and other procurement stakeholders within procurement legal frame work of the country to ensure optimal performance including provision of technical inputs to negotiation in strategic contracts.

7.    Ensure compliance with the Public Procurement Act and its regulations.

  1. Advice the Management on all issues related to procurement and disposal by tender activities of the company in compliance with the requirements prescribed under the Public Procurement Act and its regulations including any guidelines issued by PPRA from time to time.

MINIMUM EDUCATION AND EXPERIENCE:

·         Bachelor’s Degree in Procurement/ Commerce /Finance / Engineering
·         Master’s Degree in related field
·         Holder of a recognized professional certification by PSPTB
·         8 years of working experience (3 years in a senior position) 

EMPLOYMENT TERMS:

Contract of three (3) years – renewable based on performance.

Attractive remuneration package will be offered to the successful candidate.

MODE OF APPLICATION:

Applicants should submit a detailed application letter, clearly stating why you should be considered for the position, and how you will add value, a detailed curriculum vitae, and copies of certificates you wish to use in supporting your applications, three referees and two (2) passport size photographs to the address shown below. Deadline for receiving applications is 10th March, 2016

Applicants must clearly show their complete address including mobile telephone numbers and email addresses. Only shortlisted candidates will be contacted.


MANAGING DIRECTOR,
TANESCO LTD UMEME PARK,
UBUNGO P. O BOX 9024,
DAR ES SALAAM.

February 18, 2016

TAARIFA MKOA WA TEMEKE

                                       SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
     
  TAARIFA  YA LORI KUGONGA NGUZO MKOA WA TEMEKE ENEO LA KIZINGA.

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)linawataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Temeke kuwa usiku wa kuamkia leo Februari 18,2016 kuna lori limegonga nguzo ya umeme maeneo ya Mto Kizinga kwenye line ya Mbagala.Nguzo hiyo ilipogongwa iliangukia line ya maweni.Hivyo maeneo yafuatayo yanakosa umeme:

Kijichi na Maweni.Mafundi wanashughulikia kuibadilisha nguzo hiyo ambayo pia imeungua moto.

Imetolewa na ofisi ya Uhusiano,
Tanesco Makao Mkuu.

February 5, 2016

KATIZO LA UMEME MKOA WA ILALA







                                                SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
KATIZO LA UMEME MKOA WA ILALA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

SABABU:      Kubadilisha nguzo ziliizooza na matengenezo ya “Substations”  kwenye laini      ya msongo mkubwa.

MUDA:           Saa 3.00 Asubuhi - Saa 11.00 Jioni

TAREHE:      09/02/2016, Jumanne

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Tabata relini, Liwiti, Kisiwani, Kimanga, Bima, Hai bar, Ubaya Ubaya, Kisukuru, Mawenzi,
Makoka, Bonde la msimbazi, Magengeni, Beto motors, Sadolin, Five star printer, Kiwanda
cha  Guru, Kituo cha Polisi Tazara, Delta, Azania, Pepsi yundai, kiwalani bombom na
maeneo yanayozunguka. 

TAREHE:      11/02/2016, Alhamisi

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Uwanja wa ndege Terminal II, JWTZ, BP Air Port, Karakata, Semminary, Sitaki shari, Majumbasita na baadhi ya Viwanda vilivyoko barabara ya Nyerere, Metro plastic, Fusing Investment, Kiwalani kwa kalokola, Maeneo ya kwa bingubita, kwa Kapuya, Volvo, Omary packaging, Castrian, Cast steel na maeneo yanayozunguka.

TAREHE:      13/02/2016, Jumamosi

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Jangwani Romejas, Matumbi, A & B, Jangwani Sea Breeze, Shule ya Sekondari Azania, Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Upanga Kalenga, Jambo plastic, Becco, OK plastic, HTK, DT Dobi, Amary bakery, maeneo yote ya Vingunguti, Kiyembembusi, Simba, Kidarajani, PMM, Omary Packaging na maeneo yanayozunguka.


Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo, Dawati la dharura mkoa wa Ilala - 022 213 3330, 0784 768586, 0715 76 85 86, kitengo cha dharura Tabata  0684001068, 0715768589 au kituo cha miito ya simu namba 2194400 au 0768 985 100- 0684001068.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo za

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na:          OFISI YA UHUSIANO,
                                  

                               TANESCO – MAKAO MAKUU