Pages

August 31, 2016

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuwaarifu wateja wake wote wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kutakuwa na katizo la umeme, siku ya ALHAMIS tarehe 01 09/2016,saa 3:00  asubuhi mpaka 10: 00 jioni, SABABU: Matengenezo katika Kituo cha kupoza  na kusambaza umeme cha OYSTERBAY ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

MAENEO YA TAKAYO ATHIRIKA NI, Baadhi ya maeneo  ya Oysterbay, Msasani,  Kinondoni, Stanbic Bank, Ubalozi wa Kenya, Uganda Avenue, St. Peters, Leaders Club, Ada Estate, Kota za Tanesco, Ofisi za Zantel, Baby shop Msasani, Toure Drive juu pamoja na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika  toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au namba za kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100.
  
Uongozi unaomba radhi  kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na:  OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment