Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (wapili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika hilo mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, (kulia), wakati alipotembelea kituo cha
Kibeta
Wateja wakiwa wamepanga foleni kupata huduma za umeme kwenye kontena lililowekwa nje ya Ofisi za Shirika hilo mkoani Kagera, baada ya jengo hilo kuathirika vibaya
Hili ndilo jengo linalotumiwa na TANESCO kama makao makuu yake mkoani Kagera, ambalo limepata nyufa nyingi na kupelekea huduma za umeme kwa wateja kutolewa nje ya jengo hilo ambapo wateja wanaonekana wakiwa kwenye foleni
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (wapili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika hilo mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, (kulia), wakati alipotembelea kituo cha
Kibeta
Mhandisi Francis Maze
Mhansisi Mramba akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea kituo cha Kibeta
Mwangalizi msaidizi wa ofisi za Kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Misenyi
Mhandisi Mramba, na ujumbe wake wakitembelea kituo cha Misenyi
Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Mramba (kushoto), akizungumza na wafanyakazi
Na
Henry Kilasila, Bukoba
MKURUGENZI
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba,
amekagua miundombinu ya TANESCO iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi na
kuzungumza na wafanyakazi mjini Bukoba mkoani Kagera leo Septemba 16, 2016.
Karibu
jengo lote la Ofisi za Makao Makuu ya TANESCO Mkoa wa Kagera, limepata nyufa
nyingi na hivyo kuufanya Uongozi wa Shirika Mkoani Kagera, kuhamishia shughuli
zake nje ya jengo, ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wateja kwenye makontena
mawili ambayo yamewekwa nje ya Ofisi hizo.
Mhandisi
Mramba ambaye amewasili mjini Bukoba mapema leo asubuhi Septemba 16, alianza
ziara yake kwa kukagua vituo vya kupoozea na kusambaza umeme vya Kabeta, Kyaka
na Misenyi na kuzungumza na wafanyakazi.
“Nianze
kwa kuwapongeza wafanyakazi wenzangu kwa hatua za haraka mlizochukua mara baada
ya kutokea tetemeko la ardhi, kwa kuhakikisha mnazima umeme, hiyo imepelekea
kuepusha vifo ambavyo vingesababishwa na umeme wakati wa tetemeko hilo,”
Alisema Mhandisi Mramba, wakati akiongea na wafanyakazi nje ya jengo la Makao
Makuu ya TANESCO Mkoani Kagera.
Mhandisi
Mramba, pia alisema, “Baada ya kukagua vituo vyetu vya kupooza na kusambaza
umeme, tunashukuru Mungu, hakuna athari katika mifumo yetu ingawa majengo
yamepata nyufa na mengine yanahitaji kufanyiwa ukarabati wa haraka,” alsiema.
Mhandisi
Mramba pia aliwataka wafanyakazi wa TANESO, kuwasaidia wenzao waliopatwa na
athari kutokana na tetemeko hilo ambapo yeye mwenyewe alianzisha harambee na
kufanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 3.3 zikiwemo fedha taslimu na
ahadi zilichangwa.
“Sisi kama
shirika tumekwisha toa mchango wetu wa jumla kusaidia waathirika wa tetemeko
hili kupitia Msajili wa Hazina, lakini kwa vile waathirika wa tetemeko hili ni
watanzania wenzetu, ni wadau wetu wakubwa, nimeagiza ofisi zetu kote nchini
kuzungumza na wafanyakazi ili tufanye mchango kuwasaidia watanzania wenzetu.”
Alisema.
wafanyakazi hao ni Reuben Naibalema, James
Augustine, Khalima Khalid, Edson Edwin, Innocent Nyonyi na Nelson Felix.
Naye
Meneja wa TANESCO Mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, aliwapongeza
wafanyakazi wa wake kwa kufanya kazi kubwa katika kipindi chote tangu janga
hilo litokee, na kuwataka waendelee kulitumikia taifa kwa moyo wa kizalendo na
upendo.
Watu 17
walipoteza maisha, huku wengine zaidi ya 200 wakijeruhiwa na nyumba zaidi ya 5,000 zikiharibiwa na
tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha Richa 5.7 na lililotikisa umbali wa
kilomita 10 chini ya ardhi. Tetemeko hilo lilitokea majoira ya jioni ya
Septemba 10, 2016.
No comments:
Post a Comment