Pages

October 7, 2016

TANESCO, yasaini mkataba wa ujenzi 400kV utakao unganisha nchi za Kenya na Tanzania

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa Kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton baada ya kusaini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme (transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, Makao Makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. TANESCO imeingia mkataba na Makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za Kimarekani
309.26


NA HENRY KILASILA/Dar

SHIRIKA la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na Makampuni matatu kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), ya Msongo wa Kilovolti 400 njia hii ya umeme itaziunganisha Nchi za Tanzania na
 Kenya.
Hafla ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika Oktoba 7, 2016 Makao Makuu ya TANESCO Jijini Dar es Salaam, ambapo TANESCO imetiliana saini mikataba hiyo na makampuni ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na Kalpa-Taru.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi Mramba alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita 414, utaanzia Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.
Kisha Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.
“ Napenda niwahakikishie kuwa, huu ni mfululizo wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali kupitia TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Megawati 2000 katika pande zote kenya na Tanzania”. Alifafanua Mhandisi Mramba.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Mramba alsiema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26 utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2.
“Dola za Marekani Milioni 258.82, zitatumika kujenga upande wa Tanzania na  Dola za Kimarekani Milioni 50.45 zitatumika kujenga mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi Mramba.

Aidha Mhandisi Mramba aliwataka wakandarasi waliopewa kazi hiyo kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
“ Angalizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini mradi ndani ya muda kama ambavyo tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa kukamilisha ujenzi kwa mujibu wa mkataba ni kushindwa kufanya kazi na sisi, TANESCO hatutakubaliana na hilo.” Alionya Mhandisi Mramba.
Naye mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia Kandiero, alitoa hakikisho kuwa Benki hiyo itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii, kwa manufaa ya eneo lote la Afrika.
Kwa upande wake, Afisa Miradi msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, aliungana na AfDB, kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na JICA, katika kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kama huu uliosainiwa.



 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton wakisaini mkataba huo
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba
 Mhandisi Mramba, akibadilishana hati na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, baada ya kusaini mkataba.
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakisaini mkataba kutekeleza mradi huo
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakibadilishana hati
 Mkurugenzi Mkazi wa AfDB nchini, Tonia Kandiero, akizungumza kwenye hafla hiyo
 Mhandisi Mramba, (kulia) na Kandiero, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo
 Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bibi. Kandiero
 Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza
Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bi. Rosina wa JICA
 Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, akizungumza kwenye hafla hiyo
 Mratibu wa Miradi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Khalid James, (kulia), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Mramba, (wasaba kushoto), akipongezwa na Mwakilishi mkazi wa AfDB, hapa nchini, Tonia Kandiero, wakati wa picha ya pamoja na wawakilishi wa makampuni yaliyopata kandarasi ya ujenzi wa mradi huo
 Kutoka kushoto, Patrick Canton, S.K. Sarotra, Apolei Rosina, Mhandisi Mramba, Tonia Kandiero na Bisera Hadzialjevic, wakiwa katika picha ya pamoja mwishoni mwa hafla hiyo
 Afisa Mawasiliano na Uhusiano wa TANESCO, Henry Kilasila, (kualia), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Felchesmi Mramba.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (Uwekezaji), Mhandisi Decklan P.Mhaiki, akiwakaribisha wageni kwenye hafla hiyo.
Meneja mradi huo wa KTPIP, Mhandisi Mhandisi Lewanga Tesha, (kulia), akiwa na wawakilishi wa kampuni ya KALPA-TARU

No comments:

Post a Comment