Pages

May 3, 2017

Rais atoa ahadi kwa Wafanyakazi siku ya Mei Mosi





Na Magreth Subi-Moshi

Siku ya Wafanyakazi Dunia ambayo kila Mwaka huadhimishwa Mei 01, Kitaifa Mwaka huu imefanyika Mkoani Kilimanjaro katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika.na kuhudhuriwa na ma elfu ya Wafanyakazi katika Taasisi za Serikali na mashirika TANESCO ikiwa miongoni mwa Mashirika ya Serikali ambayo Wafanyakazi wake walishiriki.

Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, alifurahishwa na umoja na ukarimu uliooneshwa Wafanyakazi kutoka Mkoani Kilimanjaro na sehemu tofautitofauti Nchini na kusema haijawahi tokea.

 Mhe. Rais akiambatana na viongozi wa juu wa Serikali akiwamo Makamu wa raisi Mhe. Samia Suluhu, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika Mhe.  Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri na Wabunge.

Aidha, Mhe. Raisi, alitoa ahadi tano kwa Wafanya kazi na kusisitiza suala la makundi mawili ya  vyeti feki na vyenye utatanishi katika Taasisi mbali mabali za umma, alisema vyeti feki katika Taasisi za umma ni elfu 9000 na vyeti vyenye utatanishi ni vyeti 1500( cheti kimoja kina tumiwa na watu zaidi ya wawili).

Mbali na hayo, ahadi tano alizotoa Raisi, ni pamoja na baada ya kukamilika  suala la uhakiki wa vyeti Serikali itatoa ajira eflu 52,000 kwa Mwaka wa fedha 2017/2018 unaoanza Mwezi Julai, akiongelea Bima ya ajira alisema Serikali imeshaanza kuifanyia kazi na kuongeza kuwa Bima hiyo haitachukua nafasi ya fao la kujitoa, na kusisitiza katika suala la uhamisho na kuwaataka Wafanyakazi wote kutokubali kuhamishwa au kuhama mpaka pale watakapo patiwa  maslahi yao.

Aidha, alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejitahidi na bado inafanya jitihada kubwa kuboresha maslahi ya Wafanyakazi ili waweze kunufaika katika nyanja mbalimbali, pia aliwaambia kutakua na ongezeko la mshahara la Mwaka na kupanda kwa vyeo kwa Mwaka huu wa Fedha.

Alimalizia kwa kusema Mei Mosi ya Mwaka huu ni ya kipekee Mkoani Kilimanjaro na kwa sasa Serikali inafungua ukurasa mpya ya mahusiano baina yake na Wafanyakazi wa Tanzania na kuwataka kutimiza wajibu kazini na si maneno na unyanyasaji wa Wafanyakazi endapo atagundua Wafanyakazi wananyanyaswa hatolifumbia macho.




No comments:

Post a Comment