Pages

June 28, 2017

MOTO WAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME MKOANI RUKWA



NA MWANDISHI WETU
WATU wasiojulikana wamechoma msitu wa Kirando wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambao umeunguza miundombinu ya umeme ya Shirika la umeme Nchini TANESCO.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni hii Juni 24, 2017 na Kaimu Meneja Uhusinao wa TANESCO makao Makuu, Bi. Leila Muhaji, imesema, uharibifu huo mkubwa wa miundombinu umeathiri upatikanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo ya Kirando na Kipili wanaopata huduma ya umeme ya njia ya msongo mkubwa wa umeme unaopita kwenye maeneo hayo.
“Mafundi wa TANESCO waliofika kwenye eneo hilo, wameshuhudia uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa.” Alisema Bi Leila katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Bi Leila amesema TANESCO inawaomba wananchi wote waishio kwenye maeneo hayo kutoa taarifa kwenye ofisi za TANESCO au kituo cha polisi kilicho karibu ili kuokoa miundombinu ya umeme kwa manufaa ya taifa.
Amesema, tayari vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na TANESCO wameanza msako ili kuwabaini wahusika ili sheria ichukue mondo wake.

 Afisa wa polisi akiwa eneo la tukio huku akishuhudia jinsi moto huo ulivyoathiri nguzo za umeme

MOTO WAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME MKOANI RUKWAMOTO WAATHIRI MIUNDOMBINU YA UMEME MKOANI RUKWA

1 comment:

  1. Hey, that’s really a good post on pets for sale in Delhi, i really like your blog as the information is very useful if you are a pet lover. Well, there is one more site for the same service www.helpadya.com you should check it for more detail.

    ReplyDelete