Pages
▼
November 29, 2017
Dkt. Kalemani atembelea Viwanda vya kuzalisha nguzo Mufindi
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (Pichani Kulia) ametembelea Viwanda vya kuzalisha nguzo vilivyopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Lengo la ziara hiyo ni kujiridhisha uwezo wa Viwanda vya ndani katika kuzalisha nguzo, kwani kuna baadhi ya Wakandarasi wa REA ambao bado wanaagiza nguzo kutoka nje licha ya zuio la Serikali.
Aidha, Dkt. Kalemani, aliwataka TANESCO na REA kuwachukulia hatua Wakandarasi wanao agiza nguzo kutoka nje ya nchi kwani Viwanda vya ndani vimeonesha vinauwezo wa kuzalisha nguzo za kutosha.
Akisoma taarifa ya utoaji huduma ya umeme Wilaya ya Mufindi kwa Mhe. Waziri, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Allan Benard alisema kitanesco Wilaya inaundwa na Mji wa Mafinga, Kituo kikubwa cha kupoza umeme cha Mgololo na Ofisi ndogo ya Kijiji cha Kibao.
Aidha, TANESCO Mufindi inajumla ya Megawati 10 na matumizi ya juu ni Megawati 9.5.
Wilaya inapata umeme kutoka kwa wazalishaji binafsi kwa njia ya maji cha Mwenga Megawati 3.5.
Pia Wilaya ilitekeleza Miradi ya umeme Vijijini Awamu ya pili kwa kujenga njia ya msongo wa kilovolti 33 kutoka Makambako hadi Kwatwanga yenye urefu wa kilometa 89.7, Mafinga Igomaa kilometa 80, Nyororo mpaka Mbalamaziwa kilometa 20. na Ifwagi mpaka Mwitikilwa kilimeta 6. Jumla ya Wateja 1476 walinufaika na mradi huu.
Mhe.Waziri alitoa pongezi kwa Wafanyakazi wa TANESCO, kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana.
No comments:
Post a Comment