Pages

November 19, 2017

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani atembelea kituo cha ufuaji umeme Kidatu

Waziri wa Nishati akiongea na waandishi wa Habari alipotembelea kituo cha Kidatu

Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani ametembelea Kituo cha kufua umeme wa maji cha Kidatu (MW 204)  ambapo amekagua mashine no. 2 iliyoharibika na kuona matengenezo yake yanayoendelea kufanyika na wataalam wa TANESCO kidatu ambapo amewahakikishia wananchi kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha hakutakuwa na mgao wa umeme.

Aidha, Mhe. Waziri ameiagiza TANESCO kuhakikisha ukarabati unafanyika katika Mashine.

Mhe. Waziri amesifu juhudi za mafundi wanaoendelea na ukarabati wa mashine hiyo, na kutoa siku saba iwe inafanya kazi.







1 comment:

  1. Tanesco kazi mnayofanya inaonekana. Msikatishwe na kutishwa na wasiopenda Maendeleo ambao hawajui mfumo wa kazi zenu ama kwa sababu zao binafsi wanapotosha umma.

    Hongera sana na Poleni kwa majukumu haya mazito ya kuangaza Nchi na kuirahisisha uzalishaji wa viwanda vyetu

    ReplyDelete