Pages

December 14, 2017

Dkt. Kalemani " Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kuleta maendeleo kwa Wananchi"

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani







 
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwa katika ziara ya kukagua mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia Mkoani Mtwara, amekitembelea Kijiji cha Kalipembe kitakacho nufaika na mradi wa umeme Vijijini Awamu ya Tatu.

Kijiji hicho kipo Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, ambapo Wananchi wamekuwa wakihitaji na adha ya kutokuwa na umeme licha ya njia ya imepita kuelekea Wilaya ya Newala miaka 18.

Dkt. Kalemani akiambatana na Viongozi wa TANESCO na REA aliwahakikisha Wananchi wa Kijiji hicho kupata umeme kupitia Awamu ya Tatu ya umeme Vijijini.

"Ndugu zangu Wananchi kazi yetu ni moja tu kuhakikisha mnapata umeme,  Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kuleta maendeleo kwa Wananchi wote, bila kujali itikadi kwani suala la maendeleo halina vyama". Alisema Dkt. Kalemani.

Aidha,  alitoa maagizo kwa Mkandarasi kuanza kazi mara moja ya kuchimbia nguzo, na kuutekeleza mradi huo bila kuruka Kijiji, Kitongoji hata Kaya, ambapo Mkandarasi aliahidi kuanza kazi mapema Wiki ijayo.

Akiongelea hali ya upatikanaji wa umeme Mikoa ya Lindi na Mtwara, Dkt. Kalemani alisema hivi sasa Mkoani wa Mtwara hakuna tatizo la umeme baada ya Matengenezo kukamilika.

"Kwa Mkoa wa Lindi tumeunda tume ya watu wa tano ili kufuatilia tatizo lipo sehemu gani katika miundobonu, tunawaahidi hali kuimarika baada ya muda mfupi". Alisema Dkt. Kalemani.

Aliongeza, Mikoa ya Kusini inatarajiwa kupata suluhisho la kudumu la tatizo la umeme itakapoingizwa katika Gridi ya Taifa, ambapo mwakani Mwezi Aprili inatarajiwa kituo cha Kuzalisha umeme cha Megawati 300 kuanza kujengwa.

Dkt. Kalemani anaendelea na ziara yake ambapo amekagua kituo cha kuzalisha umeme cha Tunduru, na cha Namtumbo vilivyopo Wilaya ya Ruvuma akiwa anaelekea katika Mradi wa Makambako - Songea.






No comments:

Post a Comment