Pages
▼
January 25, 2018
Dkt. Mwinuka afanya kikao na Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Morogoro
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka amefanya kikao na Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2018.
Ikiwa ni kikao chake cha kwanza kukutana na Wafanyakazi tangu kuteuliwa kwake.
Dkt. Mwinuka alisema kukutana kati ya Uongozi na Wafanyakazi kunapunguza "Gape" na kuondoa malalamiko.
Alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Wafanyakazi wa TANESCO kwa kufanya kazi nzuri mwaka uliopita wa 2017 kwani kwa kiasi kikubwa malalamiko ya Wateja kwa Mkoa huo yalipungua na pia Mkoa wa Morogoroulitekeleza vizuri Operesheni ya KA - TA.
Akizungumzia hali ya kifedha ndani ya Shirika aliwataka Wafanyakazi kushiriki kila mmoja kuboresha kwa nafasi yake, kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kwa upaande wa vifaa vitoke stoo kwa mahesabu mazuri.
"Sehemu kubwa ya Wafanyakazi wa TANESCO ni waaminifu na wachapa kazi, lakini hao wachache wanaohujumu waache ili Wafanyakazi wote tuwe waaminifu". Alisema Dkt. Mwinuka.
Aliwataka Wafanyakazi kuongeza nguvu zaidi ili kufikia malengo.
Wafanyakazi walitoa maoni na kuuliza maswali mbalimbali ambayo Uongozi uliyatolea ufafanuzi, na yaliyo yalihitaji utekelezaji uliyapokea.
No comments:
Post a Comment