MKURUGENZI MTENDAJI TANESCO, DKT. TITO MWINUKA |
TAARIFA KWA UMMA:
FEBRUARI
10, 2020
TAHADHARI
KWA WANANCHI WANAOISHI PEMBEZONI MWA MKONDO WA MAJI YATOKAYO KWENYE VYANZO VYA KUFUA
UMEME KWA MAJI VYA MTERA NA KIDATU
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatoa tahadhari kwa Wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa mkondo wa maji yatokayo katika mabwawa ya kufua umeme kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kufuatia taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali
ya Hewa Nchini (TMA) kuwa mvua bado zinaendelea na zipo juu ya wastani, TANESCO
inafanya tathmini iwapo siku za usoni maji yahamie upande wa pili kwa ajili ya
usalama wa Mabwawa na Mitambo.
TANESCO inatoa tahadhari hii muhimu kwa Wananchi
hususani wale wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile
Uvuvi, kulisha Mifugo, Kilimo na shughuli nyingine kwenye mkondo wa mto,
vidimbwi au pembezoni mwa bwawa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu, kijamii
na kiuchumi kwa kipindi hiki ambacho mvua za Vuli zikiwa zinaendelea kunyesha.
Hali ya Ufuaji umeme katika mabwawa ya Mtera na
Kidatu unaendelea vizuri kwa asilimia mia moja (100%) na kiwango cha maji
kimeongezeka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kuanzia mita 691.22 juu ya
usawa wa bahari kuanzia Desemba 01, 2019 hadi kufikia mita 698.40 juu ya usawa
wa bahari Februari 10, 2020 katika bwawa la Mtera.
Shirika litaendelea kuhamasisha na kutoa elimu
kwa wananchi wote waishio maeneo ya pembezoni mwa mkondo wa maji na mabwawa ya
Mtera na Kidatu kwa ushirikiano na Viongozi
wa Wananchi wa maeneo hayo.
TANESCO itaendelea kutoa taarifa mara kwa mara kadri
hali ya mvua itakavyokuwa inaendelea.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO-Makao Makuu
No comments:
Post a Comment