Pages

July 14, 2020

Utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati



Miaka mitano imetimia Serikali  ya Awamu ya Tano ikiacha alama Sekta ya Nishati ambapo utekelezaji wa mradi Mkubwa wa kimkakati wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere MW 2115 unaendelea kwa kasi.

Aidha, katika mradi wa Julius  Nyerere ujenzi wa Kituo cha Kupokea na Kusambaza Umeme (Switch yard) upo katika maandalizi ya awali ambayo ni kusafisha eneo na kufanya utafiti wa udongo yamekamilika ambayo yalianza Oktoba 2019 na Mei 2020 yamekamilika kwa kulingana na mpango kazi ulivyo.

"Utafiti wa miamba na udongo umeshafanyika pia shughuli za kusafisha eneo hilo", alisema Mhandisi Eliaza Wangwe, Mtaalamu wa miamba na udongo kwenye mradi wa Julius Nyerere.

eneo la kituo cha kupokea umeme lina ukubwa wa mita za mraba 58,075 na kituo kipo umbali wa mita 450 kutoka jengo la kuendeshea mitambo ya kufua umeme.

Zabuni ya ujenzi wa Njia Kuu ya msongo wa kilovolti 400 itakayosafirisha umeme kutoka kwenye kituo hiki kuingia kwenye gridi ya Taifa imeshatangazwa.

Aidha, utekelezaji wa maeneo mengine unaendelea na upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.






No comments:

Post a Comment