Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Aprili 30, 2021
majira ya saa 4:28 usiku limefanikiwa kuwasha kituo cha kupokea na
kupoza umeme cha Dege Kigamboni.
Ujenzi
wa kituo cha kupokea umeme cha Dege umefanywa na Wataalamu wa TANESCO,
vifaa na mitambo vimeletwa na Mkandarasi Ms Telenergy d.o.o na njia ya
umeme imejengwa na Mkandarasi Kampuni ya JV Tontan Ltd Group Six.
Kuwashwa
kwa kituo hicho cha Dege kumeenda sambamba na uwashaji wa umeme kwenye
njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 132 kutoka kituo cha
Mbagala hadi cha Dege.
Kituo cha Dege kinatarajiwa kuwa mkombozi wa changamoto za umeme kwa wakazi wa Kigamboni na maeneo jirani.
Awali
wananchi wa Kigamboni walipata umeme kupitia njia ndogo ya msongo wa
kilovoti 33kV kutokea kituo cha Ilala na walikuwa wakikabiliwa na tatizo
la umeme kukatika mara kwa mara pamoja na umeme kuwa mdogo.
Baada
ya kuwasha kituo hicho umeme wa uhakika utapatikana katika maeneo yote
ya wilaya Kigamboni ikiwemo maeneo ya Kimbiji, Mwongozo, Mwasonga, Pemba
mnazi, Kisarawe2, na maeneo ya Viwanda vikubwa Wilayani hapo.
Mradi wa Dege ulianza kutekelezwa Mwezi Mei, 2019 kwa gharama ya shilingi 26.2 Bilioni.
No comments:
Post a Comment