Pages
September 26, 2021
TANESCO MPYA IMEZALIWA LEO, TUNATAKA IENDESHWE KIBIASHARA- Waziri Makamba
September 4, 2021
MIRADI YA KIMKAKATI YA NISHATI ITAKAMILIKA KWA WAKATI
Naibu Katibu Mkuu Nishati, Bw. Kheri Mahimbali amesema miradi yote ya
kimkakati ya umeme inayotekelezwa na Serikali kupitia TANESCO
itakamilika kwa wakati.
Bw. Mahimbali ameyasema hayo leo Septemba 03, 2021 katika ziara ya
Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, kukagua vituo vya kuzalisha umeme
kwa gesi vya Kinyerezi.
Amesema ziara ilijikita zaidi kwenye mradi wa Julius Nyerere, ambapo
Sekretarieti iliweza kufahamu hatua zote za kuzalisha umeme hadi
kuusafilisha.
"Leo tumewaonesha Kinyerezi complex ambayo ina Kinyerezi I, Kinyerezi I
Extension pamoja na Kinyerezi ll" amesema Bw. Mahimbila.
Ametoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inayoongozwa na Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa
inayoifanya katika kuendeleza miradi ya umeme nchini.
Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri inahitimisha leo ziara ya siku tatu
kukagua miradi ya umeme, ziara ilianzia kwenye kituo cha kupokea na
kupoza umeme cha Zuzu Jijini Dodoma, njia ya umeme itakayojengwa hadi
Chalinze na mradi wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere.
September 3, 2021
Mkandarasi JNHPP ameshalipwa trilioni 2.7
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka amesema
Mkandarasi anaetekeleza mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) Mw 2115
ameshalipwa jumla ya shilingi trilioni 2.7 kulingana na mpango kazi kati
ya shilingi trilioni 6.5 anazotakiwa kulipwa hadi kukamilika kwa mradi.
Dkt. Mwinuka ameyasema hayo leo Ijumaa Septemba 03, 2021 katika ziara ya
Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri, Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Ikulu na Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kwa upande wake Karani wa Baraza la Mawaziri, Bw. Nsubili Joshua amesema
ameongozana na Maafisa wa Sekritarieti ili kujionea kazi inavyoendelea
JNHPP.
Amesema mradi wamekuwa wakiufahamu kwenye makaratasi hivyo wamefika kujionea hali halisi na kuona kinachoendelea.
Ameongeza kuwa wameona mambo makubwa ambayo hawayajatarajia na kutoa
pongezi kwa viongozi wakuu Serikalini kwa kuutekeleza mradi huo.
Awali akieleza lengo la ziara hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya utumishi wa umma, Bw. Lauren Ndumbaru amesema wamefanya
ziara katika mradi na watumishi wa umma wa ngazi zote ili watumishi
waweze kuona na kuthamini kazi ambayo Serikali inafanya katika ujenzi wa
miradi ya kimkakati.
"Naamini kabisa mradi wa Julius Nyerere ukikamilika utaleta maendeleo
makubwa katika Nchi yetu, niombe watumishi wa umma wafanye kazi kwa bili
na waendelee kuiunga mkono Serikali ili tuone matokeo mapema" amesema
Bw. Ndumbalo
Naibu Katibu Mkuu Nishati, Bw. Kheri Mahimbali amesema Wizara ya Nishati
imefarijika kutokana na Ofisi zote mbili kuridhishwa na utekelezaji wa
mradi wa Julius Nyerere.
"Tunamshukuru Rais Samia Hassan kwa kuendelea kuuangalia mradi huu kwa
jicho la kipekee kabisa, tunapata pesa za kuendeleza mradi kwa wakati na
usimamizi mzuri, tutaendelea kuusimamia na kuhakikisha mradi huu
unakamilika kwa wakati" amesema Bw. Mahimbila.
August 19, 2021
August 18, 2021
Hatua nyingine kubwa JNHPP
Kazi ya usimikaji wa bomba (Draft tube) sehemu ya chini kabisa kwenye
mashine nambari 9 imeanza Agosti 17, 2021, katika mradi wa kufua umeme
wa Julius Nyerere (JNHPP), bomba hizo zitatumika kutolea maji katika
mitambo ya kufua umeme na kuyarudisha mto Rufiji kwa ajili ya matumizi
mengine.
Hii ni hatua kubwa iliyofikiwa baada ya kukamilika kwa uundwaji wa bomba
hizi zinazofungwa katika kitako cha msingi wa zege, kilichopo eneo la
mita 42.7 juu ya usawa wa bahari.
Usimikaji wa bomba hizi ndio utawezesha kuanza kwa ufungaji wa sehemu za
juu za mashine (turbine) na kisha jenereta za kufua umeme.
August 14, 2021
WAZIRI MKUU AKAGUA KITUO CHA TANESCO MSAMVU BAADA YA KUATHIRIKA NA MOTO
Waziri Mkuu wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa,
leo Agosti 14, 2021 amekagua kituo cha kupokea na kupoza umeme cha
Msamvu mkoani Morogoro.
Mhe. Majaliwa amekagua athari zilizotokea baada ya kupata hitilafu
iliyopelekea kuwaka moto kwa jumba la kudhibiti mifumo ya umeme wa
msongo wa kilovolti 33 Agost 2, 2021.
Aidha, amewataka Wafanyakazi wa TANESCO kuendelea kufanya kazi kwa
uaminifu na weledi kutokana na nishati ya umeme kuwa ndio injini ya
ukuaji uchumi wa Nchi.
" Watumishi wa TANESCO mmebeba mioyo ya watu, muongeze umakini katika utendaji wenu wa kazi", amesema Mhe. Majaliwa.
Katika hatua nyingine Mhe. Majaliwa ameiagiza TANESCO Kufanya mapitio ya
Wafanyakazi wanaosimamia vituo vya kupokea na kupoza umeme ili
kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi.
Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Msamvu mkoani Morogoro ni moja
kati ya vituo 51 ambavyo vinapokea na kupoza umeme mkubwa wa gridi ya
Taifa.
August 11, 2021
NAIBU KATIBU MKUU AKAGUA MRADI YA UMEME LUGURUNI
Naibu Katibu Mkuu Nishati, Bw. Kheri Mahimbali, Agosti 07, 2021 alikagua
utekelezaji wa mradi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Luguruni
Jijini Dar es Salaam.
Utekelezaji wa mradi wa Luguruni ulianza Aprili 01, 2020 na unatarajiwa
kukamilika Septemba 30, 2021 ikiwa ni miezi 18 ya utekelezaji wa mradi.
Kukamilika kwa mradi wa Luguruni kutaboresha hali ya upatikanaji wa
umeme katika Mikoa wa Pwani na Dar es salaam hasa kwa maeneo ya Kimara,
Mbezi, Hospitali ya Taifa ya Mloganzila, msigani, kibamba, kibwegere,
kisarawe, Maili moja na TAMCO (Industrial area) ambayo yamekuwa na
changamoto ya kukosekana kwa umeme wa uhakika kutokana na njia za umeme
zinanipeleka maeneo hayo kusafiri umbali mrefu.
Gharama za uzalishaji mradi wa Luguruni ni Shilingi Bilioni 15.2 ambazo
zinagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MANUFAA YA KITUO CHA UMEME DEGE KWA KIGAMBONI NA MAENEO YA JIRANI
Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Dege ni mkombozi katika kukuza
shughuli za kiuchumi na kijamii kwa Wilaya ya Kigamboni na maeneo jirani
kutokana na kuimarisha upatikanaji wa umeme baada ya kukamilika kwa
utekelezaji wake Aprili 30, 2021.
Maeneo ya Viwandani, Pemba Mnazi, Mwasonga, Mwongozo, Kimbiji na maeneo
jirani awali yalikuwa yanapata changamoto ya umeme kukatika au kuwa
mdogo kutokana na njia ya umeme kusafiri umbali mrefu kutokea Mkoa wa
kitanesco wa Ilala.
Akitembelea kituo hicho Agosti 07, 2021 Naibu Katibu Mkuu Nishati, Bw.
Kheri Mahimbali ameridhishwa na usimamizi wa kituo cha Dege ambacho
kilianza kujengwa Mei 02, 2019.
Aidha, mahitaji ya sasa ya Wilaya ya Kigamboni ni megawati 18 huku uwezo
wa kituo cha Dege ni megawati 48 lakini malengo ya Serikali ni
kukiongezea uwezo hadi hadi kufikia megawati 96.
August 10, 2021
TANESCO NA STAMICO WASAINI UTEKELEZAJI MRADI WA MAKAA YA MAWE KIWIRA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) leo Agosti 10, 2021, limesaini hati
ya makubaliano na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuhusu
utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 200 kwa kutumia
makaa ya mawe ya Kiwira.
Akiongea wakati wa uwekaji saini Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito
Mwinuka amesema utekelezaji wa mradi wa Kiwira utaenda sambamba na
ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme kutoka ya urefu wa km 100 kutoka
Kiwira hadi kituo cha kupokea umeme cha Mwakibete Mbeya.
Aliongeza kuwa, kwasababu mradi unagusa Taasisi mbili ni vyema kuwa na hati ya makubaliano ili kufahamu jukumu la kila Taasisi.
"STAMICO na TANESCO ni wadau wa mradi wa Kiwira, kwa maana kwamba
STAMICO wao wanahusika na mgodi wa makaa ya mawe, TANESCO tutasimamia
ujenzi wa mtambo wa kufua umeme", alisema Dkt. Mwinuka.
Amesema utekelezaji wa mradi wa Kiwira umeambatana na faida nyingi kwa
Nchi ikiwemo uwepo umeme wa kutosha na kuweza kufanya biashara na Nchi
jirani.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji STAMICO, Dkt. Venance Mwase amesema jukumu kubwa la STAMICO ni uchimbaji wa madini.
Serikali imekuwa ikisisitiza umuhimu wa Taasisi za Serikali kushirikiana
katika miradi mbalimbali ya maendeleo na hata kutoa huduma.
"Siku hii ya leo tumefikia makubaliano na TANESCO katika kuuendeleza mradi wa Kiwira kwa manufaa ya Taifa ", alisema Dkt. Mwase.
July 1, 2021
TANESCO YAENDELEA KUIMARISHA MFUMO WA LUKU
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka Juni 29, 2021
akizungumza na vyombo vya habari katika Ofisi za TANESCO Mikocheni
Jijini Dar es Salaam amesema kuwa, kazi ya kuimarisha mfumo wa kuuza
umeme wa malipo ya kabla (LUKU) bado inaendelea na maboresho ili
kuimarisha zaidi uwezo wa mfumo huo kwa kuuongeza mfumo mbadala
(backup).
Dkt. Mwinuka ameyasema hayo alipokutana na Waandishi wa habari kutolea
ufafanuzi jinsi TANESCO inavyojipanga kuondokana na changamoto ya
kukosekana kwa mfumo wa manunuzi ya umeme pamoja na ongezeko kubwa la
mahitaji ya umeme nchini.
Aidha, Dkt. Mwinuka ameongeza kuwa, mfumo huo wa LUKU ulianza kufanya
kazi Mei 19, 2021 mchana baada ya kutokea kwa hitlafu ya manunuzi ya
umeme Mei 17 na 18, 2021 na hivi sasa kazi ya kujenga mfumo mbadala
inaendelea.
"Hivi sasa tunaendelea na kazi ya kuhamisha taarifa kutoka kwenye mfumo
wa msingi kupeleka kwenye mfumo mbadala baada ya kuukamilisha kuujenga"
amesema Dkt. Mwinuka.
Ameongeza kuwa, katika kipindi hiki cha maboresho ya mfumo kutakuwa na
changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika manunuzi ya umeme
kutokana na majaribio katika mfumo mbadala.
Amesema iwapo wananchi wanapata changamoto ya kununua umeme kupitia
mtandao mmoja, ni vyema kutumia mtandao mwingine pamoja na huduma za
kibenki.
June 28, 2021
June 27, 2021
TANESCO YAWEZESHA MATIBABU MOI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limechangia kiasi cha Shilingi
Milioni Ishirini kwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), ili kusaidia na
kuwezesha matibabu ya watoto wenye vibiongo katika hospitali hiyo.
Akiongea katika Mbio fupi za kuchangia matibabu hayo (Moi marathoni)
Juni 27,2021, katika viwanja vya chuo cha udaktari Muhimbili MUHAS,
Meneja uhusiano wa TANESCO, Bi. Johary Kachwamba amesema kuwa TANESCO
imeona umuhimu wa kurudisha kwa jamii sehemu ya kile inachokipata
kupitia mauzo ya Umeme kwa kusaidia matibabu ya watoto hao.
"TANESCO imeamua kuangaza maisha ya jamii yetu kwa namna ya tofauti,
tunafarijika kwamba matibabu haya yataokao uhai na kurejesha furaha kwa
watoto wenye vibiongo" amesema Bi. Kachwamba
Sambamba na kuchangia kiasi hicho, wafanyakazi wa TANESCO pia
wameshiriki katika kukimbia mbio hizo katika makundi ya km 5, km 10 na
km 21, ambapo mshindi wa tatu mbio za km 5, kwa upande wa Wanaume ni Bw.
Sebastian Kwayu, kutoka TANESCO.
Mgeni Rasmi aliepoke hundi kwa niaba ya MOI katika tukio hilo ni, Mhe.
Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
ambapo alitoa shukrani kwa wote waliochangia ikiwa ni pamoja na TANESCO.
May 26, 2021
TANZANIA YAPATA DOLA MILIONI 140 UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME MARAGARASI
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO, leo Mei
26,2021, imeingia makubaliano ya mkopo wa Dola milioni 140 kutoka Benki
ya Maendeleo ya Africa (ADB) kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kufua
umeme wa megawati 49.5 kupitia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi
uliopo Mkoani Kigoma.
Mradi wa Maragalasi utachochea ukuwaji wa shughuli za maendeleo ya
kijamii pamoja na kiuchumi kwa wakazi wa Mikoa ya Kaskazini Mashariki
mwa Tanzania.
Mradi huu, utahusisha pia uimarishaji gridi ya Taifa itakayorahisisha
biashara ya mauziano ya Nishati ya umeme baina ya Tanzania na Nchi
majirani.
Aidha gharama za mradi huo kwa ujumla ni takriban Dola milioni 144.14,
ambapo Serikali ya Tanzania itachangia kiwango kinachobakia cha Dola
milioni 4.14 kukamilisha fedha za Ujenzi wa Mradi huo muhimu kwa Mikoa
ya ukanda wa Kaskazini Mashariki na Tanzania kwa ujumla.
May 1, 2021
KITUO CHA UMEME KIGAMBONI CHAKAMILIKA
April 27, 2021
WATAALAMU TANESCO KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI