Pages

February 21, 2012

Hivi ndivyo vishoka na wafanyakazi wa TANESCO wasio waaminifu wanavyohujumu shirika letu (TANESCO)





Hii ni mita iliyotumika ambayo haikusajiliwa 
na TANESCO..





Maafisa wa Polisi kutoka Kituo cha Kati wakishirikiana na Maafisa Usalama wa Tanesco mkoa wa Temeke, wamefanikiwa kuzibaini nyumba mbili zilizounganishiwa umeme kinyemela na kujenga nguzo tisa kwa kutumia vishoka katika la Vigozi lililoko Mbagala jijini Dar es Salaam.


Mmoja wa maafisa wa Polisi waliofanikisha zoezi hilo Afande Sospeter Antony, wa Kituo cha Kati, aliwata wamiliki wa nyumba hizo kuwa ni Mr. Ibrahim Mohammed Nyingila pamoja na Bw. Said Rajab anayefanya kazi Mamlaka ya Bandari.

Hujuma hii dhidi ya Tanesco iligundulika baada ya raia wema kutoa taarifa za kitendo hicho kwa kikosi kazi cha kupambana na hujuma za namna hii, kilicho chini ya Afande Sospeter na Maafisa Usalama wa Tanesco.

Baada ya kuhojiwa na maafisa wa usalama, wamiliki wa nyumba hizo kwa nyakati tofauti walikiri kujipatia huduma ya umeme kinyume na utaratibu, kwa kulipa zaidi ya milioni kumi kama malipo ya ujenzi wa nguzo tisa kwa Vishoka, ambao hata hivyo majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.

Walipotakiwa kuelezea ni namna gani nguzo hizo zilifika katika eneo hilo, wamiliki hao walisema  zililetwa na gari la Tanesco ambalo hata hivyo hawakufanikiwa kushika namba zake za usajili.

Katika utafiti uliofanywa na maafisa wa Tanesco, waligundua kuwa nguzo zote, nyaya na mita zilizotumika katika kutekeleza hujuma hiyo ni mali ya Tanesco.

Aidha nyumba hizo zilikutwa na mita ambazo hazikujasajiriwa, na hivyo kutumia umeme pasi na kuulipia.
Baada Maafisa Usalama kuchukua vielelezo, mafundi wa TANESCO walizichomoa nyaya zote kutoka kwenye nguzo, na taratibu za kisheria zinaendelea.



Kulia ni nguzo waliyochukulia umeme 
na kushoto ni nguzo ya kwanza katika tisa zilizojenga 
na vishoka


 Hii ndiyo nguzo ya kwanza kati ya 
tisa iliyowekwa pasi utaratibu wa TANESCO 
na vishoka

SHIRIKA LIMEWEKA MIKAKATI MAALUMU KUKOMESHA VISHOKA NA WAFANYAKAZI WANAOSHIRIKI KATIKA WIZI WA UMEME.

SHIRIKA LINAWAPONGEZA WALE WOTE WANAOTAMBUA UMUHIMU WA NISHATI HII ADHIMU KWA MAENDELEO YA WATANZANIA WOTE, NA KWAMBA KULINDA MALI NA MIUNDOMBINU YAKE NI WAJIBU WETU SOTE. KWA HUDUMA YA UMEME FIKA KATIKA OFISI ZA TANESCO NA HAKIKISHA UNAPATA RISITI KWA MALIPO YOYOTE UTAKAYOFANYA


No comments:

Post a Comment