UFAFANUZI KUHUSU UAMUZI WA MAHAKAMA KUU KUHUSIANA NA
SHAURI KATI YA TANESCO NA DOWANS.
Kufuatia uamuzi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya ombi la TANESCO kukata
rufaa juu ya pingamizi lililowasilishwa na Dowans dhidi ya ombi la TANESCO,
kumekuwa na taarifa sisizo sahihi zilizoandikwa aidha kwa kutokufahamu au kwa
sababu zingine na kutangazwa na baadhi
ya vyombo vya habari ambazo TANESCO inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
- TANESCO iliwasilisha ombi la kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama kuu uliotolewa na Jaji Emilian Mushi tarehe 28 Septemba, 2011 ambao uliamuru pamoja na mambo mengine uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICC) usajiliwe rasmi na mahakama ya hapa Tanzania.
- Aidha, kwa mujibu wa taratibu za rufaa TANESCO iliomba ruhusa (leave to appeal) toka Mahakama Kuu ili iruhusiwe kuwasilisha rufaa yake rasmi mbele ya Mahakama ya Rufaa Tanzania.
- Sanjari na ombi la ruhusa, TANESCO iliwasilisha ombi la kuitaka Mahakama Kuu isitishe kukaza hukumu ( application for stay of execution) ya tozo ya ICC kama ilivyoamriwa tarehe 28 Septemba 2011 na Mahakama Kuu.
- Dowans kwa upande wake waliwasilisha pingamizi dhidi ya ombi la TANESCO la kukata rufaa kwa madai kuwa uamuzi wa ICC kama ulivyoridhiwa na Mahakama Kuu haukatiwi rufaa, kwa mujibu wa sheria
Tarehe 20 Februari, 2012, Mahakama Kuu kitengo cha biashara chini ya Jaji Dk.
Fauz Twalib ilitolea uamuzi maombi
ya TANESCO hali kadhalika pingamizi la
Dowans kama ifuatavyo;
1.
Pingamizi lililowekwa na DOWANS dhidi ya TANESCO
lilikuwa halina sababu ya kuwepo kwa kuwa TANESCO wana haki ya kisheria kupinga
maamuzi ya ICC kama yalivyoridhiwa na Mahakama Kuu katika Mahakama ya Rufaa.
Pingamizi hilo lilitupiliwa mbali.
2.
Ombi la kukata rufaa lililowasilishwa na
TANESCO lilionekana kuwa si la lazima kwa vile TANESCO tayari walikuwa na haki ya
kisheria kukata rufaa .
3.
Kuhusu ombi la kusitishwa kukaziwa hukumu kama
lilivyowasilishwa na TANESCO, Mahakama iliamuru ombi hilo lisikilizwe tarehe 18 April 2012
Tunaomba vyombo vya habari kuwa makini wakati wa kuripoti
taarifa ya kesi hii kati ya DOWANS na TANESCO ili kuepuka upotoshwaji ambao kwa
namna moja au nyingine huenda ukaleta tafsiri tofauti na ukweli wa maamuzi ya
mahakama.
Badra Masoud
Meneja Mawasiliano
No comments:
Post a Comment