Pages

March 3, 2012


Mwili wa Bw. GODLISTEN baada ya kupigwa shoti 
ambayo ilisababisha kifo 
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Godlisten, amefariki dunia kwa kupigwa shoti ya umeme, akituhumiwa kujaribu kuiba mafuta ya transifoma, iliyoko katika Kituo kikuu cha mabasi, Arusha mjini.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano kwa wateja  TANESCO Mkoa wa Arusha, Bw. Benedict Nkini, mtu huyu akufanikiwa kuharibu chochote katika transifoma kwani alipigwa shoti na kufa hapo hapo akiwa katika harakati za kuiba mafuta ambayo hata hivyo hakufanikiwa hata kufunguwa sehemu za kutolea mafuta.
 
Hii ndio transfoma, na sehemu ya nguo ya Bw. Godlisten .




No comments:

Post a Comment