Pages

March 3, 2012

TUNAOMBA RADHI KWA WATEJA WETU


Shirika la Umeme Tanzania  – TANESCO linapenda kuwaomba radhi wateja wake wote wanaoishi maeneo ya Gongo la mboto, Ukonga, Segerea, Moshi Bar, Kipunguni,  Mazizini, Kisarawe, Pugu Mikongeni,Pugu Kajiungeni,Chanika,Markaz,Chuo Cha Kampala, Ukonga Magereza, Majohe, Kiwanda cha Namera, Tabata Kisiwani, Tabata Kisukulu, Bonyokwa, Tabata Segerea, Tabata Kinyerezi, Tabata Bima, Tabata Chang’ombe, Karakata, Stakishari, Kisarawe na baadhi ya Maeneo ya viwanda vilivyopo  kandokando ya barabara ya Mandela hadi Mwananchi kutokana na tatizo la kukatikakatika kwa umeme kwenye maeneo hayo.

Tatizo hilo limesababishwa na kuharibika kwa transfoma kubwa iliyoko katika kituo chetu cha umeme cha Kipawa iliyokuwa inasambaza umeme kwenye maeneo hayo.Tatizo hilo lilipelekea kutumia njia mbadala ya kusambazia umeme ya kutoka Ubungo badala ya ile ya awali ya Kipawa ambayo kuanzia mwezi wa Januari, 2012 hadi sasa imezidiwa kutokana na ongezeko kubwa la matumizi ya umeme. Mikakati ya dharura ya kulishughulikia tatizo hilo inaendelea ikiwa ni pamoja na kukarabati njia hiyo ya kusambazia umeme kwa kuimarisha maungio,kubadilisha nguzo zilizooza na kukata matawi ya miti yanayoizonga njia hiyo.

Pia ujenzi wa njia mpya unaendelea ili kuhamisha wateja wa kisarawe na Gongo la Mboto kupata umeme kupitia kituo cha Ilala.Mikakati ya muda mrefu ni pamoja na kushughulikia upatikanaji wa transfoma kubwa ya Kipawa na upanuzi wa kituo hicho.
Kwa msaada na  matukio ya dharura tafadhali piga simu namba zifuatazo:-
022 213 3330, 0784 768586, 0715 768586 ofisi ya mkoa Ilala, 0715 76 85 84 au 0688 00 10 71 ofisi ya wilaya ya Gongo la Mboto, 0684 00 10 68 ofisi ya wilaya ya Tabata na 0684 001066 ofisi ya wilaya ya viwandani. Nama za kituo cha huduma kwa wateja (Call centre numbers) 2194400 au 0768 985 100
Shirika linasikitika kwa usumbufu wowote unaojitokeza kutokana na tatizo hili.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu




1 comment:

  1. Tanesco pls help,umeme unekatika hapa home tangu jana naomba msaada 0772 88 33 88

    ReplyDelete