HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI
TANGAZO
Mkurugenzi wa TANESCO anawatangazia ndugu na jamaa wa Marehemu waliozikwa kwenye Makaburi yaliyopo ndani ya eneo la mradi wa upanuzi wa njia za umeme Kata ya Manzese, Mtaa wa Midizini na Kata ya Ubungo Mtaa wa Ubungo Kisiwani kwamba anakusudia kuhamisha Makaburi hayo 250 ili shughuli ya upanuzi wa njia ya umeme iweze kuanza.
Kwa mujibu wa Sheria za mitaa (Mamlaka za Miji) ya mwaka 1982, kanuni ya mwaka 2008 namba 46(c) Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itasimamia zoezi hili kwa kutumia wataalam wake.
Taarifa inatolewa kuwa watu wote wenye ndugu au jamaa waliozikwa kwenye eneo hilo wafike Ofisi za Afisa Mtendaji wa Kata za Manzese na Ubungo kujiandikisha wakiwa na barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Mtaa anaoishi kabla ya tarehe 25/07/2013.
Makaburi hayo yatahamishiwa kwenye Makaburi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yaliyoko Tegeta Kata ya Kunduchi baada ya taratibu zote kukamilika.
(Imesainiwa na)
Eng. Mussa Natty
Mkurugenzi wa Manispaa
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI
Pages
▼
June 28, 2013
June 20, 2013
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AKIZUNGUMZA NA UONGOZI WA KAMPUNI ZA UMEME MAREKANI.
Waziri wa nishati na madini Mh.Prof.Sospeter Muhongo akizungumza na uongozi wa kampuni za umeme za marekani za symbion na General Electric (GE) katika ukumbi wa wizara hiyo juu ya ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme wa MW 400 mkoani Mtwara.
June 19, 2013
TAHADHARI WIZI WA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA
TAHADHARI WIZI WA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA
Kwa masikitiko makubwa, Shirika la Umeme Tanzania - TANESCO linasikitishwa na vitendo vinavyoendelea vya kuhujumu miundombinu ya Shirika ikiwepo kuibiwa nyaya za umeme huko Arusha mwezi mmoja uliopita, kuibiwa kwa vyuma vya nguzo huko Morogoro na siku ya Jumapili Juni 16, 2013 kuibiwa mafuta pamoja na winding za transfoma iliyopo Mbezi Kibamba kwa Tendwa jijini Dar es Salaam. Wizi huu unatokea wakati Shirika linajitahidi kuboresha huduma zake kote nchini.
Kutokana na wizi huo, wateja zaidi ya 150 waliathirika kwa kukosa umeme tangu Jumapili hadi jana jioni Juni 17, 2013 ambapo Shirika ilibidi litafute na kufunga Transfoma nyingine ambayo ilikuwa imepangwa itumike kusambaza umeme kwa wateja wengine ambao hawajawahi kupata huduma ya umeme kabisa.
Uongozi wa Shirika unasikitika kwa vitendo hivi na unawaomba wananchi wote kutoa taarifa Polisi au Ofisi zozote za TANESCO zilizopo karibu nao wanapoona watu wanaowatilia shaka kutaka au kuhujumu miundombinu ya Shirika.
Au wasiliana nasi, Kituo cha Miito simu namba 2194400 au 0786985100
"Tuilinde Miundombinu ya TANESCO kwa maendeleo yetu na Taifa kwa ujumla"
Imetolewa na:
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.
June 13, 2013
TAARIFA KUHUSU KATIZO LA UMEME MKOA WA TANGA
TAARIFA KUHUSU KATIZO LA UMEME MKOA WA TANGA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tanga linasikitika kuwataarifu wateja wake wa wilayani za Korogwe, Handeni, Lushoto na Muheza kwamba kutakuwa na makatizo ya umeme siku ya Jumamosi Juni 15, 2013 na Jumapili Juni 16,2013 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Sababu ni kufanya matengenezo muhimu katika laini zinazoingia na kutoka katika Kituo kipya cha sambaza umeme cha Songa. Maeneo yatakayoathirika ni: Wilaya yote ya Korogwe isipokuwa maeneo ya Hale, Segera, Michungwani, Kabuku, Mkata, Kwachaga hadi Manga. Wilaya yote ya Handeni, Wilaya yote ya Lushoto na, Wilaya yote ya Muheza Tafadhali usiguse waya ulidondoka au uliokatika, toa taarifa Ofisi yoyote ya TANESCO iliyokaribu nawe. Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tanga linasikitika kuwataarifu wateja wake wa wilayani za Korogwe, Handeni, Lushoto na Muheza kwamba kutakuwa na makatizo ya umeme siku ya Jumamosi Juni 15, 2013 na Jumapili Juni 16,2013 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Sababu ni kufanya matengenezo muhimu katika laini zinazoingia na kutoka katika Kituo kipya cha sambaza umeme cha Songa. Maeneo yatakayoathirika ni: Wilaya yote ya Korogwe isipokuwa maeneo ya Hale, Segera, Michungwani, Kabuku, Mkata, Kwachaga hadi Manga. Wilaya yote ya Handeni, Wilaya yote ya Lushoto na, Wilaya yote ya Muheza Tafadhali usiguse waya ulidondoka au uliokatika, toa taarifa Ofisi yoyote ya TANESCO iliyokaribu nawe. Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU
June 7, 2013
KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANI
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu
wateja wake wa Mkoa wa Pwani kuwa kutakuwa na katizo la umeme Siku ya Jumamosi,
08 Juni, 2013 kuanzia Saa 03:00 Asubuhi hadi 10:00 jioni. SABABU
ni Kufanya matengenezo, kubadilisha nguzo zilizooza katika
Line ya Msongo wa 33KV
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Mlandizi, Kongowe, Visiga, Kwa Mathias, Kwa Mfipa, Picha ya Ndege, Maili
Moja, Miembe Saba, Kiluvya, Soga na maeneo yanayozunguka.
Tafadhali usiguse waya wowote uliokatika. Mwananchi
usikate mti unaogusa au kukaribia line toa taarifa TANESCO kupitia namba No. 0232402850,
0655989935; 0688359998 au Call Centre No. 2194400 OR 0786985100
Uongozi
unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.
TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – MKOA WA DODOMA
TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – MKOA WA DODOMA
Shirika
la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika
kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Dodoma
kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-
TAREHE: 16/06/2013; Jumapili
SAA: 3:00 Asubuhi - 12:00 Jioni
SABABU:
KUWEZESHA KUUNGANISHWA KWA CIRCUIT
BREAKER MPYA KATIKA KITUO CHA KUPOOZEA UMEME CHA MSONGO UMEME WA 220/33KV CHA
ZUZU NA KUUNGANISHA KITUO KIPYA CHA MSONGO UMEME WA 33/11KV,10MWA CHA MZAKWE
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
VISIMA
VYA MAJI VYA MZAKWE, VYEYULA, MAKUTOPOLA JKT, MSALATO, MIPANGO, MIYUJI,
MAILIMBILI, CHANG’OMBE, CHINANGALI, CHAMWINO, AREA A, AREA C, AIRPORT, UHINDINI
HOSPITALI
YA MKOA, JAMATINI, UZUNGUNI, MLIMA WA IMAGI, MAKULU, KILIMANI, GEREZA LA
ISANGA, HOSPITALI YA MILEMBE, NZUGUNI
CBE, MAKOLE,
VETA, OFISI ZA BUNGE, CHADULU, SWASWA, AREA D, MARTIN LUTHER, IPAGALA
UDOM, KISASA,
HOMBOLO, IHUMWA, MAENEO YOTE YA WILAYA ZA BAHI, CHAMWINO, KONGWA, MPWAPWA, NA
GAIRO na maeneo yote yanayozunguka.
Tafadhali
usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo: 026 2321728, 0732961270,
au Call centre namba 2194400
au 0768 985 100
Uongozi
unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na: Ofisi ya Mawasiliano,
TANESCO – Makao
Makuu.
June 5, 2013
TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI
na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwataarifu Wateja
wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa katizo la umeme kama
ifuatavyo:-
TAREHE:
06/06/2013 (Alhamisi)
SAA: 3:00
Asubuhi hadi saa 11:00 Jioni.
SABABU: Matengenezo katika laini ya msongo mkubwa,
Kubadilisha nguzo zilizooza na
kukata Miti.
MAENEO
YATAKAYOATHIRIKA:
Tegeta CCM, Chanika, Njia panda ya wazo
factory, Tegeta Masaiti, Tegeta Namanga, Boko Basihaya, Boko CCM, Boko
Maliasili, Boko National Housing, Ndege beach, Mbweni Kijijini, nyumba 151 za
Serikali/Mh.Magufuli, Bakili Muluzi school, kwa Kala mweusi, Mbweni Mpiji, Kota
za Wazo, Dogodogo centre, uwanja wa Nyuki, Ofisi ya Raisi flats, Marando street
Bunju, Presidents Office Mbweni, Mbweni Kijijini, and Mabwepande na baadhi ya
maeneo ya Bagamoyo.
Tafadhali kuwa makini na nyaya za umeme
zilizo chini. Ukiwa na wasiwasi piga simu Usishike waya wa umeme TANESCO Tegeta: 0717 650878, 0688
650878 au Kinondoni Kaskazini: 022
2700367, 0784 768584, na 0716
768584 Au namba za huduma kwa wateja 022-2194400 au 0768 985 100.
Uongozi
unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa
na: OFISI
YA UHUSIANO,
TANESCO –
MAKAO MAKUU.