Pages

August 27, 2013

MKOA WA KINONDONI KASKAZINI

TAARIFA YA UFUNGUZI WA OFISI MPYA – MBEZI BEACH
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linayo furaha kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa Shirika limefungua ofisi mpya ya Wilaya ya MBEZI BEACH iliyopo maeneo ya Tangi Bovu ilipokuwa Supermarket ya IMALASEKO. Ofisi itahudumia wateja wa maeneo ya Mbezi Beach yote, Goba, Kunduchi, Salasala, Afrikana na Kilongawima.
HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA SASA NI:-
·     Kupokea maombi ya awali
·     Huduma za dharura
·     Uunganishwaji wa huduma ya umeme na
·     Huduma zote za kiufundi
TANESCO inaendelea na jitihada za kukusogezea huduma zake pale ulipo. Kwa mawasiliano zaidi piga namba zifuatazo: 022 2700367, 0784 768584, 0716 768584. Au Kituo cha Miito namba 2194400.
IMETOLEWA NA:  OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

2 comments:

  1. Mimi naishi mivumoni shule ya secondari waya waumeme wajilani yangu umegusajuu ya batilangu naombeni msaada wenu muje kuamisha mahana niatari 0654097029

    ReplyDelete
  2. Waya waumeme umegusa juu ya bati langu naombeni msaada mjekuamisha mahana niatari nipo mivumoni 0654097029

    ReplyDelete