Pages

September 9, 2013

ARUSHA NA KILIMANJARO

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMATANO 11/09/20123 na IJUMAA 13/09/2013 kuanzia saa 8:00 Asubuhi – 12:00 Jioni.  Sababu ni kubadilisha nguzo zilizooza eneo la Kambi ya Mkaa.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Kilimanjaro International Airport, Sakila, eneo la Machimbo ya Mawe njia panda ya KIA, Sanya Juu, Boma Ng’ombe, Wilaya za Hai na Siha na maeneo yanayozunguka maeneo hayo.
Tafadhali: usiguse wala kusogelea waya wa umeme uliokatika toa taarifa TANESCO Kwa waya uliokatika (simu: 0732979280, 2506110 na 2503551/3).
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
IMETOLEWA NA:- OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment