Pages

September 26, 2013

MWANZA

KATIZO LA UMEME MKOA WA MWANZA NA WILAYA YA GEITA.
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Mwanza na wilaya ya Geita, kuwa kutakuwepo na katizo la umeme SIKU YA JUMAMOSI YA TAREHE 28/09/2013 kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 12.00 JIONI.
SABABU YA KATIZO HILI NI MATENGENEZO KWENYE KITUO KIPYA CHA KUPOKELEA UMEME KILICHOJENGWA NA MRADI WA MCC KILICHOPO NYASAKA NA KUBADILISHA NGUZO ZILIZOOZA KATIKA ENEO LA IBANDA.
Maeneo yatakayoathirika na katizo hili ni NYASAKA,MAJANINI,NATIONAL,BAADHI YA MAENEO YA MABATINI,FURAHA BAKERY,MWATEX,MECCO,NYAKATO FOOD, NYAKATO MWANANCHI,BUZURUGA, BUSWELU, KANGAE,SIMA, IGAKA, ISUNGANHOLO, KASAMWA,SARAGULWA, CHIGUNGA, CHIKOBE,BUKONDO NA GEITA MJINI.
TAHADHARI
Tafadhali usishike,usikanyage wala kusogelea nyaya za umeme zilizolala chini ,unaweza kuwasiliana  na kitengo  cha  dharura TANESCO Mwanza  kupitia  namba zifuatazo 028 250 0090 , 028 250 1060.
SHIRIKA LINAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
                        Imetolewa na:    Ofisi ya Uhusiano.
                                                   Tanesco:MakaoMakuu                                         

No comments:

Post a Comment