Pages

October 2, 2013

DODOMA

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA DODOMA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa
wa Dodoma kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI tarehe 05/10/2013
kuanzia saa 03:00 Asubuhi hadi saa 10:00 Jioni.   Sababu ni kubadilisha nguzo
zilizochakaa.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:-
Wilaya ya Kondoa – Aya Sekondari, Mondo, Kelema Maziwa, Dalai, Jenjeluse, Goima, Songolo, Hamai, Churuku na maeneo yanayozunguka.
Wilaya ya Kiteto – Chamanda, Mrijo Juu, Mrijo Chini, Soya, Kiteto Mjini, Mapango, Matui, Dosidosi, Engusero, Njoro, Chekanao, Kipelesa na maeneo yote ya Kiteto
TAFADHALI USIGUSE WALA KUKANYAGA NYAYA ZILIZOANGUKA, toa taarifa kupitia namba zifuatazo:-  namba za dharura Mkoa wa Dodoma 026 2321728, Wilaya ya Kondoa 0767114047, Wilaya ya Kiteto 0767902380 na 0732961274. au namba za kituo cha huduma kwa wateja 2194400 or 0768 985 100.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:    OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment