Pages

October 15, 2013

KATIZO LA UMEME MKOA WA MWANZA


Shirika la Umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Mwanza, linasikitika kuwataarifu wateja wake kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya Alhamisi Oktoba 17, 2013   kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

 

SABABU:

Kubadilisha nguzo zilizooza kwenye njia ya kusafirishia umeme kwenda wilaya ya Magu, maeneo ya Butimba na Nyegezi.

 

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:-

Nyanguge, Lugeye, Kahangara, Iungu, Magu Mjini, Nsola, Masanzakona, Sogesca, Mwamanyili, Nasa, Nyashimo, Bulima, Nyashimo,  Mwanangi, Kasoli Ginnery, Mkuyuni (Chakechake na Shede), Butimba, Magereza Butimba, Butimba TTC, Chuo cha Sauti, Malimbe, Nsumba Sec, Nganza Sec, Iseni Nyegezi Fisheries na Mashine za Maji Nyegezi.

 

 

TAHADHARI

Tafadhali usishike, usikanyage wala kusogelea nyaya za umeme zilizolala chini, wasiliana  na kitengo  cha  dharura TANESCO Mwanza  kupitia   namba 028 250 0090 au 028 250 1060.

 

SHIRIKA LINAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

 

 

Imetolewa na:  OFISI YA UHUSIANO

                           TANESCO MAKAO MAKUU.    

 

1 comment: