Pages

November 18, 2013

VIWANDA NA MIGODI

TAARIFA KWA UMMA

Wakati matengenezo ya kiufundi katika visima vya gesi vilivyopo katika kisiwa cha Songosongo, wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi yakiendelea na kusababisha upungufu wa umeme katika gridi ya taifa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linawaomba wateja wake wenye viwanda na migodi kusitisha matumizi ya umeme nyakati za usiku na kuendelea kutumia umeme nyakati za mchana tu ili umeme uweze kutosheleza wateja wa majumbani katika kipindi cha usiku.

Zoezi hili ni la muda mfupi kuanzia sasa hadi Novemba 26, mwaka huu ambapo matengenezo ya kiufundi katika visima hivyo vya gesi yatakuwa yamekamilika na umeme kurejea katika hali ya kawaida.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU 

1 comment:

  1. Tanesco

    Dont you think such maintenance should be done during the cool months like June/July to spare Dar Residents of scorching heat? can you use gas only for few months to let water build up in dams and use hydro during such days when gas is not available?

    ReplyDelete