Pages

December 16, 2013

OPERESHENI YA UKUSANYAJI WA MADENI YA UMEME



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake na wananchi wote kwa Mikoa yote nchini kulipia madeni yao ya umeme waliyolimbikiza hadi Novemba 2013. Wateja Binafsi, Mashirika ya Umma na Idara za Serikali zenye madeni ya umeme hadi kufikia mwezi Novemba 2013 wanatangaziwa kuwa watasitishiwa huduma ya umeme ifikapo Desemba 20, 2013 bila taarifa (Notisi) ya ziada.
Wateja wanaodaiwa wanatakiwa kulipia Ankara zao za umeme kuepuka usumbufu katika kipindi hiki cha Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya.
TAHADHARI:
USISOGELEE WALA KUKANYAGA WAYA ULIOKATIKA WAJULISHE TANESCO KWENYE OFISI ILIYO KARIBU au PIGA SIMU NAMBA: 0768985100/+255222194400.

LIMETOLEWA NA:  OFISI YA UHUSIANO           
 TANESCO MAKAO MAKUU     

No comments:

Post a Comment