Pages

December 12, 2013

Katizo la umeme mkoa wa Kinondoni Kusini



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI tarehe 14/12/2013 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi 11:00 jioni.  Sababu ni kujenga laini ya msongo mkubwa ili kuboresha upatikanaji wa umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Stendi ya mabasi Ubungo, TBS, Dar Brew, Ubungo Sisimizi, Sinza ukuta wa Posta, Ubungo Plaza, Shekilango, TBL Ubungo depot, Pan Afrika, Ubungo NHC, Twiga cement Ubungo depot na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo  0222171762 – 65, 0784271461, 0715271461,  Au Call centre number 2194400 or 0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na:  OFISI YA UHUSIANO,
                            TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment