Pages

April 30, 2014

Wahandisi TANESCO waokoa bil. 12.7



Wahandisi na Mafundi Mchundo wa Kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia cha Ubungo Gas Plant 1, wamefanikisha ukarabati mkubwa wa mitambo ya Kituo hicho bila kutumia mkandarasi
wa nje au wa ndani na hivyo kuokoa kiasi cha TZS bil. 12.7 ambazo zingelipwa kama kaziWahandisi TANESCO waokoa bil. 12.7 hiyo ingetangazwa zabuni.

Akizungumzia mafanikio hayo Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Ambakisye Mbangula alisema
Wahandisi na Mafundi Mchundo hao wameweza kufanya ukarabati mkubwakatika mashne hizo za kufua umeme baada ya kufanyakazikwa saa 16,000.Kituo hicho chenye uwezo wa kufua megawati
104, kilikabidhiwa TANESCO baada ya mkandarasi kumaliza mkataba wake wa kukijenga Desemba 04, 2011.

Kumbukumbuku zinaonesha kuwa mkandarasi alishawahi kufanya ukarabati mkubwa kwa gharama ya Euro 460,150 sawa na shilingi za kitanzania1,056,981,037.2 kwa mashine moja. Hivyo kwa mashine zote 12 mkandarasi angelipwa pesa ya kitanzaia 12,683,772,446.4 sawa na euro 5,521,800.

Mhandisi Mbangula alisema kituo hicho kilizinduliwa rasmi No vemba 04, 2008 na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanza kufua umeme kibiashara Julai 30, 2007 kwa kushirikisha Wahandisi wazawa wa TANESCO na WARTISILA. Kituo cha Ubungo (1) kilijengwa
ili kuongeza vyanzo vya kufua umeme ili kuondoa utegemezi wa maji. Kituo kinafua umeme kwa kutumia gesi asilia kutoka visiwa vya Songo Songo wilaya Kilwa Mkoani Lindi chini ya usimamizi
wa kampuni ya PAN AFRICA.

Jumla ya shilingi bilioni 99.45 zilitolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na mwaka 2006 mitambo ilianza kufungwa na kampuni ya WARTSILA kutoka Finland.

“Kituo kina mashine 12, kila mashine moja inauwezo wa kufua megawati 8.73. Mashine zote zinauwezowa kufua jumla ya megawati 104. Baada ya mradi kukamilika yalifanyika majaribio katika mitamboambapo zilipatikana megwati 102 ambazo kituo kinazalisha hadi sasa ikiwa ni pungufu ya megawati2, upungufu huo unatokana na umbali kutoka usawa wa bahari,joto pamoja na unyevu unyevu” alieleza Mhandisi Mbangula.

Kiasi cha bar 50 mpaka 70 cha gesi husafirishwa kutoka Songo Songo ambapo hupunguzwa mpaka
bar 5 ambazo huingia kwenye mashine kwa ajili ya kufua umeme. Mhandisi Mbangula alisema wafanyakazi wahandisi na mafundi mchundo walipata mafunzo kwa wakati mradi unajengwa nchini Finland, Singapore na Italia.

Mkuu wa Kitengo cha Matengenezo Mhandisi Nimrod Nderingo kwa upande wake ameeleza umuhimu wa kufanya ukarabati wa mashine kwa wakati. Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha uendeshaji mitambo Mhandisi Abdallah Abeid alisema

Mhandisi Nimrod Nderingo akitoa maelekezo kuhusiana na mfumo wa ufuajiumeme kwa njia ya gesi unavyofanya kazi mitambo hiyo inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa kwa kutumia mifumo ya kompyuta na iwapo itatokea hitilafu yoyote katika mitambo huonekana katika komputa. Pia mitambo inaweza kuzimwa ama kuwashwa kwa kutumia komputa. Aliwataka watu wenye mawazo kuwa TANESCO inafanya kazi kizamani kubadili mitazamo yao kwani Shirika linaendana na teknolojia za kisasa.

Kwa mujibu wa Afisa Rasilimali Watu wa kituo hicho Bi. Getrude Chandika kuna jumla ya wafanyakazi hamsini na tano, kati yao wanaume ni arobaini na saba na wanawake nane. Wapo pia wafanyakazi wa muda maalum (STE) sita ambapo watano ni wanaume na mmoja mwanamke.

No comments:

Post a Comment