Pages

May 23, 2014

MKOA WA ILALA

KATIZO LA  UMEME – MKOA WA ILALA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa ILALA kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI tarehe 24/05/2014 na JUMAPILI tarehe 25/05/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi 12:00 jioni.  Sababu ni kuhamisha njia ya msongo mkubwa wa umeme kwenye maeneo ya makutano ya barabara eneo la Kamata na kubadilisha waya kwenye njia ya msongo mkubwa wa umeme ya F-I.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI
TAREHE 24/05/14
Maeneo ya mtaa wa Lugoda, Msimbazi/Makamba, Muheza, Lindi, Likoma, maeneo ya Kidongo chekundu, Kamata, Gerezani, Central police, water front, Bandari, City garden restaurant, maeneo ya uwanja wa ndege, Banana, Vingunguti, TAZARA na maeneo mengine ya jirani.
TAREHE 25/05/14
Maeneo ya uwanja wa ndege, TAZARA, baadhi ya viwanda vilivyopo kando kando ya barabara ya Mwl. Nyerere, Vingunguti na maeneo mengine ya jirani yanayopata umeme kutoka kwenye njia ya umeme ya F I.
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka, toa taarifa kupitia simu namba: 025 250 4219, 0757 529380
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:- OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.
 

No comments:

Post a Comment