Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) linafuraha kuwajulisha wateja wake kote nchini wanaotumia
mfumo wa LUKU kwamba kuanzia Agosti 1 mwaka huu tutahamia kwenye mfumo mpya wa
LUKU ulioboreshwa zaidi.
Mfumo huo ambao
umeboreshwa utakuwa na kasi zaidi, utaweza kuhudumia idadi kubwa ya wateja kwa
wakati mmoja na utaondoa usumbufu wowote ambao ulijitokeza kwenye mfumo wa
awali.
Hivyo wakati wa kuhamia
kwenye mfumo huo mpya tutasitisha huduma ya kununua umeme kwa wateja wa LUKU usiku
wa kuamkia Agosti 1, 2015 kwa muda wa saa 24.
Uongozi unaomba radhi
kwa usumbufu wowote ambao unaweza kujitokeza.
TANESCO:
“Tunayaangaza Maisha Yako”
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU
No comments:
Post a Comment