TAARIFA YA KUKOSEKANA
KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA FEBRUARI 7, 2016
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa
mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma, Mara, Babati, Simiyu na
baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga kuwa yatakosa umeme
siku ya JUMAPILI tarehe 7 FEBRUARI, 2016 kuanzia Saa 1:00 Asubuhi hadi Saa 11.00 Jioni.
Sababu ni kazi inayoendelea kufanywa na Mkandarasi anayejenga njia kuu
ya kusafirisha umeme ya msongo mkubwa wa kilovoti 400, maarufu kama ‘Backbone’
kutoka Iringa kwenda Shinyanga.
Mradi huo unalenga kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini na
utekelezaji wake upo katika hatua za mwisho.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na: OFISI YA
UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO
MAKUU.
No comments:
Post a Comment